NIJUZE NIJUZE Author
Title: Newcastle nambari tatu sasa!
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Mabao matatu kutoka kwa mshambulizi matata Demba Ba kuliiwezesha Newcastle kuendeleza rekodi yake ya kutoshindwa katika ligi ya Premier ya U...

Mabao matatu kutoka kwa mshambulizi matata Demba Ba kuliiwezesha Newcastle kuendeleza rekodi yake ya kutoshindwa katika ligi ya Premier ya Uingereza msimu huu.

Demba Ba baada ya kuifungia Newcastle bao

Ushindi huyo wa jumatatu usiku kumuipandisha Newcastle hadi nafasi ya tatu wakiwa na jumla ya alama 22 baada ya kucheza mara kumi. Chalsea ambayo mwishoni mwa juma walifungwa na Arsenal mabao 5-3 wameshuka hadi nafasi ya nne.

Demba Ba ambaye ni mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Senegal alifunga bao la kwanza katika dakika ya 12 baada ya kupata pasi safi kutoka kwa Gabriel Obertan. Na kukiwa kumesalia dakika tano tu kipindi cha pili kumalizika ,Ba alifanya mambo kuwa 2-0.

Hata hivyo nusura Ba aharibu siku yake pale alipoisababishia Newcastle kuadhibiwa kwa mkwaju wa penalti baada ya kumsukuma Peter Crouch katika eneo la hatari.

Lakini Ba aliongoza bao la tatu katika dakika ya 81 nae kwa njia ya penalti.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top