NIJUZE NIJUZE Author
Title: Wachimbaji wadogo 5,000 watimuliwa Geita
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Uongozi wa Serikali katika wilaya ya Geita mkoani Mwanza, umewataka wachimbaji wadogowadogo katika eneo hilo kuondoka kwenye maeneo ya Mgodi...

Uongozi wa Serikali katika wilaya ya Geita mkoani Mwanza, umewataka wachimbaji wadogowadogo katika eneo hilo kuondoka kwenye maeneo ya Mgodi wa Meru wanakochimba madini ya dhahabu, ili kupisha taratibu za kisheria juu ya umiliki wa eneo hilo.

Eneo hilo lililogundulika kutapakaa dhahabu au lugha nyingine ¡¥gold rush¡¦ katika siku za hivi karibuni, limevutia wachimbaji wengi katika wakati ambao Kampuni kubwa la uchimbaji la Meru limedai kuwa na umiliki wa eneo hilo.

Kwa mujibu wa mkuu wa wilaya ya Geita Philemon Shelutete, wachimbaji hao walitakiwa kuwa wameshaondoka tangu muda wa mwisho uliowekwa juzi Jumanne jioni, kwa kuwa suala la umiliki wa eneo hilo liko mahakamani.

Amewataka wachimbaji hao kuwa watulivu katika wakati huu suala hilo linaposhughulikiwa, na kueleza kuwa baada ya eneo hilo kugundulika kuwa na dhahabu nyingi (gold rush), uchimbaji ulianza moja kwa moja bila kuzingatia umiliki.

Wimbi la wachimbaji wadogo kuhamishwa katika maeneo wanayoyagundua kuwa na madini limekuwa likiwakumba mara kwa mara, ambapo katika sakata hili haikufahamika mara moja kuwa ufumbuzi utapatikana baada ya muda gani, na hatma yao itakuwa lini.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top