NIJUZE NIJUZE Author
Title: Je utamaduni wa Kimasai kwa wanawake uendelezwe?
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Binadamu ni kiumbe tofauti sana na viumbe wengine wote waliowahi kuishi duniani. Ana akili, utashi na fikra ambazo si tu zinamuwezesha kutam...

Binadamu ni kiumbe tofauti sana na viumbe wengine wote waliowahi kuishi duniani. Ana akili, utashi na fikra ambazo si tu zinamuwezesha kutambua jema na baya, bali pia humfanya kubuni na kuchanganua mambo yanayomhusu na yasiyomhusu japo wengi hufanya hivyo kwa lengo la kujiletea maendeleo.

imageWahenga wanasema “ukiona chaelea basi ujue kimeundwa”. Ndivyo anavyohaha binadamu kuhakikisha anaunda na anayefanikiwa ni yule anayefikiri kifasaha, kubuni kwa maarifa na kuweka juhudi mbele. Ndiyo maana tunaona wengine wana maisha mazuri kwa kuwa na mahitaji bora kama nyumba nzuri, magari na hata mali nyingine.

Pamoja na kwamba inawezekana wengine hujipatia mali hizo au hali hiyo nzuri kwa njia za mkato, lakini kwa ujumla anayefanikiwani yule anayefikiri vizuri na kuweka juhudi mbele.

Binadamu huyuhuyu hupenda kujinufaisha kwa mambo mbalilimbali, na wengine hujikuta wakipitiliza hasa kwa tamaa zao kuwakandamiza wenzao kwa lengo tu la kujistawisha.

Mila na desturi zetu humtambua na kumheshimu kila mtu na hakuna mwenye mamlaka juu ya mwenzake kijamii, japo hapo zamani wanaume walihisi kuwa na haki kamili ya kiutawala juu ya mwanamke jambo lililohalalisha ulipwaji wa mahari ya kutosha wakati wa kuoa ili kumtumia mwanamke huyo apendavyo.

Enzi hizi japo si kwa ujumla, wengi wameshatambua kuwa wote tu sawa na tunapaswa kuheshimiana. Pamoja na ustaarabu huo kuna baadhi ya makabila ambayo wanawake wamekuwa wahanga wa vitendo visivyovumilika kutoka kwa waume zao.

Ni hivi karibuni tu tumesikia malalamiko kutoka kwa wanawake wa Kimasi juu ya unyanyasaji wanaoupata kutoka kwa waume zao.

Wanaume hao wamekuwa wakizihama familia zao wakiwa na mifugo kwa kisingizio cha kwenda kutafuta malisho kumbe ndo wanaondoka moja kwa moja. Wanaondoka bila kujali ukubwa wa familia hizo na pia zitakuwa zinaishi vipi kimatumizi. Ikumbukwe mifugo ndiyo chanzo pekee cha uzalishaji na kipato kwa kabila hilo.

Pamoja na dhahma nyingine wanazokumbana nazo, alisikika mwana mama mmoja akisema “akishaondoka anaoa na akishaoa mabinti, basi sisi tunabakia tu kama mifugo na anatuambia mkipenda nendeni mnakotaka sina kazi na ninyi” alieleza mama huyo.

Kumbuka mama huyu ana watoto wakubwa hadi wadogo na wake wenza pia, hivyo kazi ya utunzaji yote huwa yake. Anakokwenda mwanaume hapajulikani kwani mbuga ni nyingi na huweza kuvuka hata mipaka ya mikoa yao na hivyo kurudi yaweza kuwa ndoto, kwani huoa upya mabinti na pengine akihama tena huanzisha tena familia nyingine.

“Huu mji umekuwa kimya tumebaki wanawake tu wanaume wote wameondoka, tunaomba Serikali itusaidie mikopo ili tuweze kujikimu,” alieleza mama mwingine kwa masikitiko.

Je, ni busara kuuacha utamaduni huu kustawi? Watoto waliozaliwa watakuwa wa nani? Na wanawake hawa wataishi vipi? Hebu fikiria mtu anaoa tena wanawake wawili, watatu, wanne na kuwazalisha watoto wa kutosha kisha anahama kuanzisha familia nyingine bila kujali ile aliyoiacha itaishi vipi, tutafika?

Pengine huu ni utaratibu wa mila zao, lakini wengi wameeleza kuwa kwa kawaida tangu zamani baba anapohama na mifugo kutafuta malisho, basi huhama na familia nzima na kuanzisha makazi mapya na sio kuitelekeza na kuoa wengine. “Mambo yamebadilika sasa, hatuangaliwi, tumetupwa” alilalamika mama huyo.

Kuna haja ya kueneza elimu sehemu hizi na kufanya pia juhudi za kupeleka sheria za kijamii (za ndoa) ili kuwabana wanaume hawa la sivyo basi tutazidi kuwa na watoto wengi tegemezi, majonzi mengi kwa wakina mama na pia njaa kwani hadi sasa kwa mfano tumeshaanza kusikia watu wakihitaji msaada wa chakula katika mikoa ya Arusha na Manyara jambo ambalo si kawaida kwa mikoa hiyo kukumbwa na njaa

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top