NIJUZE NIJUZE Author
Title: MGOGORO WA ARDHI MKWAYA–LINDI HATARI TUPU
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Mkwaya ni kijiji kilichopo katika manispaa ya Lindi katika Kata ya Mingoyo, kijiji hicho kipo kwenye mgogoro mkubwa wa ardhi kwa sasa. wanad...

DSC00327Mkwaya ni kijiji kilichopo katika manispaa ya Lindi katika Kata ya Mingoyo, kijiji hicho kipo kwenye mgogoro mkubwa wa ardhi kwa sasa. wanadai kupokonywa ardhi na mwekezaji Ndg: Durubai ambaye kwa sasa ndiye mmiliki wa eneo hilo tangu hapo nyuma na alikuwa anatumia eneo hilo kwa shughuli za kilimo kwa kuwakodisha wananchi hao hao.

DSC00329Wananchi wamezinduka na kudai uhalali wa mwekezaji huyo kwani wamefuatilia wamegundua mwekezaji huyo hana hakimiliki ya eneo hilo lote kwa mwaka 1958-62 eneo hilo lilikuwa chini ya mmiliki ndugu POPATI sasa wananchi wanauliza je POPATI na DURUBAI wote walikuwa wamiliki kwa wakati mmoja. swali hilo lilijitokeza katika mkutano wa hadhara kati ya wananchi hao na mh.DC wa manispaa ya Lindi lakini majibu haya kupatika. Na katika mkutano huo haukufanikiwa kwani muafaka haukupatikana kupelekea mkutano kuvunjika.

ZIARA YA MH. MBUNGE WA JIMBO LA LINDI

DSC00337Mh. Halfani Barwan alifanya ziara yake kama kawaida yake ya kutembelea maeneo yote ya jimbo lake na alifika mkwaya na kufanya mkutano wa ndani yaani Halmashauri ya Kijiji na kufuatia mkutano wa hadhara kwa wananchi wote na kuwapa rai yake juu ya kutatua suala hilo

 DSC00330na kuwaambia ni vyema kufuata sheria ilikumilikishwa kisheria ili hapo baadae isije kuwa tabu kuliko kutumia uamuzi wa kuvamia eneo na kujigawia kiholela eneo hilo hivyo basi waunde kamati ya watu 11 ambayo itaongozwa na yeye mwenyewe ili kufuatilia kwa karibu suala hilo. Wananchi walikubaliana na ombi hilo lakini walibakia na msimamo wa kugawana kwanza na ufuatiliaji baadae. Ilikulinda amani na utulivu lazima busara itumike ili kunusuru machafuko kutukea vyombo vya usalama vitazame suala hili kwa umakini wa hali ya juu kwani kama tujuavyo migogoro ya Ardhi ni jambo zito na Hatari sana hivyo washirikiane kwa pamoja ilikufikia muafaka. Maneno hayo yalitolewa na Katibu wa Ziara ya mbunge ndugu Madebe.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top