NIJUZE NIJUZE Author
Title: Umoja wa Mataifa washambuliwa Nigeria
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Kikundi cha waislamu wenye msimamo mkali nchini Nigeria - Boko Haram - kimedai kuhusika na shambulio dhidi ya makao makuu ya Umoja wa mata...

Kikundi cha waislamu wenye msimamo mkali nchini Nigeria - Boko Haram - kimedai kuhusika na shambulio dhidi ya makao makuu ya Umoja wa mataifa katika jiji la Abuja.imageMsemaji wa kundi hilo alitoa madai hayo alipoongea kwa simu na afisi za BBC nchini Nigeria. Kikundi hicho kilifanya mashambulio kama hayo dhidi ya makao makuu ya polisi mjini Abuja mwezi Juni mwaka huu. Mkuu wa polisi wa Abuja Mike Zuokumor aliwaambia waandishi wa habari kwamba mshambuliaji aliyejitoa mhanga alifariki dunia papo hapo kwani mlipuko huo ulimkata vipande vipande. Umoja wa Mataifa umesema kumekuwa na shambulio la bomu katika jengo la Umoja wa Mataifa nchini katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja. Mwandishi wa BBC Bashir Sa'ad Abdullahi ambaye alikuwepo katika eneo la mlipuko amesema ghorofa ya chini ya jengo hilo imeharibika sana. Huduma za dharura zinaondoa miili ya watu kutoka katika jengo hilo huku majeruhi wengine wakipelekwa hospitali, Makundi ya wanamgambo wa Kiislam wamekuwa wakifanya mashambulio katika jiji hilo katika siku za hivi karibuni.

About Author

Advertisement

 
Top