
Mtaa wa Azikiwe katikati ya Jiji la Dar es Salaam, ambao kawaida unakuwa na msongamano wa magari unaonekana ukiwa wazi baada ya magari kupungua mjini, kutokana na uhaba wa mafuta ya petroli na dezeli. Serikali leo imetoa karipio kali kwa baadhi ya wamiliki wa vituo vya mafuta waiogoma na wametakiwa wajieleze ni kwa nini wameamua kufanya hivyo lasivyo watachuliwa hatua za kisheria. Tamko hilo rasmi la Serikali limetolewa jioni hii bungeni na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngereja.

Eneo la mataa ya TAZARA nalo likiwa limepungua magari kwa kiasi kikubwa leo asubuhi