NIJUZE NIJUZE Author
Title: IOC yahakikisha usalama Olympiki 2012
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) imesisitiza "inahakika na kiwango cha juu" usalama katika michezo ya Olimpiki itakayofanyika...

Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) imesisitiza "inahakika na kiwango cha juu" usalama katika michezo ya Olimpiki itakayofanyika London mwaka 2012.

image

London imekumbwa na ghasia kwa siku tatu mfululizo huku maduka yakiporwa na majengo kuchomwa moto.

Msemaji wa IOC amesema suala la usalama linapewa umuhimu mkubwa, lakini si jukumu lao moja kwa moja.

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Chama cha Olimpiki cha Uingereza (BOA) Darryl Seibel, amesema anahakika michezo hiyo itafanyika na kumalizika kwa usalama.

Seibel ameongeza kusema hafahamu lolote kama kuna sehemu yoyote ya uwanja wa Olimpiki iliharibiwa wakati wa ghasia hizo.

"Hii sio taaswira ya London, hii inaonesha hali halisi ilivyo katika dunia tunayoishi nyakati hizi."

Msemaji wa michezo ya London ya mwaka 2012 amesema hatua za usalama zinaendelea kuangaliwa upya kila mara.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top