Msaada wafikia raia Somalia

image

Shirika la Msalaba Mwekundu limeweza kufikisha chakula kwenye eneo moja kati ya yale yaliyoathirika vibaya sana na ukame nchini Somalia.

Kwa kushirikiana na tawi lake katika eneo hilo, Shirika hilo lilisafirisha chakula cha watu elfu-24, kwa malori hadi eneo ambalo linadhibitiwa na na wapiganaji wa Kiislamu, al-Shabab.

Msaada huo, unaohitajika sana, ulipelekwa mji wa Baardhere kaskazini magharibi mwa mji mkuu wa Mogadishu.

Hata hivyo Shirika la chakula duniani, World Food Programme, limesema kuwa halitaweza kuwafikia watu 2.2 milioni walio ndani ya Somalia.

Msaada huo ulijumiuisha maharagwe, mchele na mafuta na umekadiriwa kuwasaida raia wa eneo hilo kwa mda wa mwezi mmoja.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post