
Mwimbaji maarufu mwanamke wa Uingereza, Amy Winehouse(27), amepatikana amekufa katika fleti yake mjini London
Amy Winehouse alishinda tuzo kadha kwa albamu yake ya pili, Back to Black, ambayo ilitolewa mwaka wa 2006.
Sababu ya kifo haijulikani bado.
Lakini mwimbaji huyo amekuwa akipambana na uraibu wa ulevi na mihadarati kwa muda.
Mara nyingi alitokeza kwenye tamasha huku amelewa