NIJUZE NIJUZE Author
Title: Mau Mau ruksa kuishitaki Uingereza
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Mahakama kuu ya Uingereza imetoa ruhusa kwa watu wanne raia wa Kenya kuishtaki serikali ya Uingereza kwa tuhuma za ukatili uliofanywa wakat...

image

Mahakama kuu ya Uingereza imetoa ruhusa kwa watu wanne raia wa Kenya kuishtaki serikali ya Uingereza kwa tuhuma za ukatili uliofanywa wakati wa ukoloni.

Wizara ya mambo ya nje pamoja na ofisi ya Jumuiya ya Madola zilisema haziwezi kubeba jukumu hilo kisheria, lakini jaji anayesikiliza shuri hilo alitupilia mbali hoja hiyo. Jaji huyo amesema hajaona kama kulikuwa na utesaji wowote, lakini kama ulikuwepo, serikali ya Uingereza ndio ilikuwa na mamlaka.

Shauri hilo litaruhusu kufunguliwa kwa kesi ya tuhuma za ukatili uliofanywa dhidi ya vuguvugu la Maumau kati ya mwaka 1952 hadi 1961.

Maumau

Waliowasilisha shauri hilo ni Ndiku Mutwiwa Mutua, Paulo Muoka Nzili, Wambugu Wa Nyingi na Jane Muthoni Mara, ambao umri wao ni kati ya miaka 70 hadi 80. Wanne hao hata hivyo hawakuwepo mahakamani.

Maumau

Katika shauri hilo, awali, jaji aliambiwa kuwa Bw Mutua na Bw Nzili walihasiwa, Bw Nyingi alipigwa hadi kupoteza fahamu katika tukio ambalo watu 11 walipigwa hadi kufa, huku Bibi Mara akinyanyaswa kijinsia. Lakini ofisi ya mambo ya nje ilisema jukumu la kisheria lilikabidhiwa kwa jamhuri ya Kenya baada ya kupata uhuru wake mwaka 1963.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top