Unknown Unknown Author
Title: ROSE MHANDO AINGIA MITINI KATIKA TAMASHA LA UIMBAJI, MASASI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Viongozi wa Dini akiwemo Askofu Oscar Mnung’a wa Dayosisi ya kanisa la Anglikan Newala akiambatana na Katibu mtendaji wa Dayosisi ya Masasi ...

SAM_0540Viongozi wa Dini akiwemo Askofu Oscar Mnung’a wa Dayosisi
ya kanisa la Anglikan Newala akiambatana na Katibu mtendaji wa
Dayosisi ya Masasi Rev Canon James Almas walilazimika kutoa tamko kwa mashabiki waliojitokeza na kutaka kila mmoja arudishiwe pesa yake hali ambayo ilikwenda kwa Amani
SAM_0517Washabiki waliohudhuria tamasha hilo katika viwanja
vya boma masasiSAM_0568SAM_0518
SAM_0562kikundi cha kwaya toka Mkuti Masasi

Na Abdulaziz -Masasi
Umoja wa akina mama wa kikristo Masasi(UMAKI)Umesikitishwa na kitendo cha Mwanamuziki wa Injili Rose Mhando Kutohudhuria Tamasha la Uimbaji lililokuwa na lengo la kukusanya pesa kwa ajili ya Ujenzi wa kituo cha watoto Yatima Masasi huku tayari Umoja huo ukiwa umekamilisha mikataba yote ikiwa pamoja na malipo.

Kutohudhuria kwa mwimbaji huyo kulileta tafrani kwa mashabiki
waliokuwa tayari wamechangia hali iliyosababisha waandaaji kurudisha pesa walizoanza kukusanya kufuatia hakikisho lililotolewa na Meneja wa Mwanamuziki huyo Bw Nathan Wami

Akizungumza na mtandao huu, Mchungaji Carlos Raphael Marcus-Makamu wa Askofu Dayosisi ya Masasi alieleza kuwa kufuatia taarifa za kutohudhuria walimtafuta Rose Mhando Kwa njia ya Simu na kukiri kupata taarifa za mwaliko huo kupitia kwa meneja wake Nathan siku 2 kabla ya Tamasha hilo lakini tayari alikuwa na Mwaliko mwingine Katika Tamasha huko Babati na kuwakikishia yupo BABATI

Sisi tulikamilisha malipo tuliyokubaliana ya Tshs Milioni nne ambazo
tulilipa kwa awamu mbili na stakabadhi tunazo kuhakikisha kufanya
hivyo na ilivyotokea tulimtafuta Nathan nae alituomba radhi na
kutuomba tumpe njia ya kurudisha fedha kitu ambacho tu nakaa kikao
kujadili kwa kuwa tumepata hasara kubwa iliyosababishwa na yeye.

Alisisitiza Mchungaji Marcus Hasara ni kubwa kwa kuwa maandalizi yalikuwa zaidi ya miezi mitano,Matangazo mengi tumeyafanya na tulilazimika kufungua kesi katika kituo cha polisi Masasi

Kufuatia hali hiyo ya kutokea kwa Mwimbaji Rose MHANDO Katika viwanja vya Boma Masasi,Viongozi wa Dini akiwemo Askofu Oscar Mnung’a wa Dayosisi ya kanisa la Anglikan Newala akiambatana na Katibu mtendaji wa Dayosisi ya Masasi Rev Canon James Almas walilazimika kutoa tamko kwa mashabiki waliojitokeza na kutaka kila mmoja arudishiwe pesa yake hali ambayo ilikwenda kwa Amani licha ya mashabiki wengi kusikitishwa na kitendo huku Tamasha likiendelea kwa kwaya mbalimbali kutumbiza katika viwanja hivyo.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top