Na Fungwa Kilozo
Wanachama Fatuma Maumba na Ahmad Mmow kutoka klabu ya waandishi wa habari wa mkoa wa Lindi wametunukiwa tuzo ya wanahabari bora wa habari za korosho kwa msimu wa 2024/2025.
Waandishi hao ambao ni wanachama wa klabu ya waandishi wa habari wa mkoa wa Lindi (Lindi Regional Press Club) walishinda na kukabidhiwa tuzo hizo jana tarehe 22.08.2025, jijini Dodoma wakati wa mkutano wa wadau wa tasnia ya korosho ambao uliandaliwa na Bodi ya Korosho Tanzania (CBT). Ambao mgeni rasmi alikuwa waziri wa kilimo, Mheshimiwa Hussein Bashe(Mb).
Kwaupande wake Fatuma Maumba ambae pia ni mwenyekiti wa klabu hiyo alipata tuzo hiyo kupitia kundi la waandishi wa runinga(TV). Ambapo Ahmad Mmow ambae ni katibu mkuu wa klabu hiyo alipata tuzo kupitia kundi la magazeti.
Mbali na makundi hayo katika tasnia ya habari lakini pia kulikuwa na kundi la wanahabari wa redio na mitandao ya kijamii. Ambapo kila kundi lilikuwa na washindani watatu ambao walipenya katika hatua za mchujo.
Kwa upande wa Radio. Mwandishi wa Rufiji FM kutoka mkoa wa Pwani alipata tuzo. Ambapo kwa mitandao, mwandishi Mohamed Kemkem kutoka Mtwara alishinda.
Mkutano huo ulifanyika jijini Dodoma katika ukumbi wa mikutano wa Morena. Ambao uliwashirikisha wadau wa zao la korosho kutoka katika mikoa 19 inayozalisha zao hilo hapa nchini.
