Hatimaye baada ya safari ngumu Yanga SC imefanikiwa kupata kile ambacho walidhamiria kukipata. Haikuwa safari nyepesi kutokana na aina ya wapinzani ambao walikutana nao.
Ushindi wa jana dhidi ya Club Africain umerejesha faraja na matumaini yaliyoingiwa na ukungu wa matokeo hafifu kwenye mechi kadhaa za mwisho za kimataifa.
Ilikuwa safari iliyojaa ndoto za walio wengi baada ya uwekezaji mkubwa kufanyika ndani ya klabu hiyo ili kufanikisha malengo yote ambayo kwa miaka mingi yalififia.
Katika mashindano haya ya shirikisho, Kwa mara ya kwanza Yanga ilikutana na El Merreikh ya Sudan mwaka 2007 ambapo walipata sare tasa wakiwa wenyeji. Na kulitolewa hatua za awali
Yanga ndio klabu ya kwanza kutoka Tanzania kuwahi kufuzu kwenye kombe la Shirikisho barani Afrika hatua ya Makundi ambapo walifanya hivyo mwaka 2016.
Vile vile wanashikilia rekodi ya kutinga hatua ya makundi ya Shirikisho ikiwa ni mara ya tatu wanaweka rekodi ambayo hakuna klabu Tanzania imefanya hivyo, wakifanya hivyo mwaka 2016, 2018 na 2022
Tokea 2007 mpaka sasa wamecheza michezo 28, wakishinda michezo 7, wakitoka sare michezo 6 na kupoteza michezo 15.
Jana ilikuwa kwa mara ya pili kwenda nchini Tunisia kwenye mashindano ya kimataifa kwani mwaka 2007 walikutana na Esperance de Tunis ambao ni mahasimu wa Club Africain ambapo mchezo wa awali walitoka sare tasa kabla ya kupoteza magoli matatu jijini Tunis.
Huu ni ushindi wa kwanza na wa kihistoria kwa klabu ya Yanga kushinda katika ukanda wa kaskazini hususani mataifa ya kiarabu.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.