Zaidi ya vijana ELFU NNE (4,000) kutoka mikoa ya Lindi, Arusha, Dodoma, Kilimanjaro na Manyara wanatarajia kunufaika na Mafunzo katika vyuo vya VETA katika mikoa hiyo kupitia program ya Ajira na ujuzi kwa maendeleo ya Afrika (E4D).
Kabongo Mbuyi, Kiongozi wa mradi wa E4D akitoa hutuba mara baada ya Makabidhiano ya vifaa vya mafunzo katika chuo cha VETA - Lindi. |
Hayo yameelezwa na kiongozi wa mradi wa program ya Ajira na ujuzi kwa maendeleo ya Afrika (E4D) Kabongo Mbuyi wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa vya mafunzo kwa wizara ya elimu, Sayansi na teknolojia yaliyofanyika katika chuo cha ufundi stadi VETA mkoani Lindi.
Makabidhiano hayo yaliyoenda
sambamba na utiaji saini makubaliano kati ya shirika la maendeleo la ujerumani
GiZ na Mamlaka ya elimu na mafunzo stadi VETA , ambapo Mbuyi amesema Program hiyo ya
E4D inalenga kukuza ajira endelevu na kuboresha hali za ajira kupitia
ushirikiano mpana wa sekta ya elimu za umma na binafsi hasa katika kukuza ajira
kwenye sekta za Ujenzi na matengenezo, nishati mbadala pamoja na utalii,
Awali kaimu mkurugenzi mkuu wa VETA ,Felix Staki alisema utekelezaji wa mradi huo katika chuo cha VETA Lindi na vyuo vingine utachangia kwa kiasi kikubwa katika kuongeza udahili, kutoa fursa zaidi ,kuimarisha ubora wa mafunzo ya ufundi stadi kwa kuwa chuo kimapata vifaa vya kisasa vya kufundishia pamoja na kuongeza ujuzi kwa walimu wa ufundi stadi kupitia kipengele cha T.O.T, huku mkuu wa mkoa wa Lindi Zainabu Tellack akisema ni matarajio ya Serikali kuona watoto watakaomaliza mafunzo hayo watakuwa na ujuzi wa kutosha utakaowawezesha kushindana kwenye soko la Ajira.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.