NIJUZE NIJUZE Author
Title: SIMBA YAIRARUA MTIBWA SUGAR 5-0 NBC PL
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
  BAADA ya kushindwa kupata bao ndani ya dakika 180 kinara wa mabao Simba, Moses Phiri amefunga bao lake la tano na kutoa pasi moja ya bao t...

 

BAADA ya kushindwa kupata bao ndani ya dakika 180 kinara wa mabao Simba, Moses Phiri amefunga bao lake la tano na kutoa pasi moja ya bao timu yake ikiibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Mtibwa Sugar mchezo wa Ligi Kuu NBC.

Mabao mawili ya Sakho, Okrah, Mzamiru na Phiri wakifunga moja moja yameipa Simba pointi tatu muhimu na kuishusha Mtibwa katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi hiyo.

Simba imecheza mchezo dakika zote 90 wakionyesha ubora maeneo yote na uchu wa kufunga mabao zaidi pamoja na kufunga mabao dakika za mwanzo za mchezo.

simbasctanzania-313100167-510462544065477-3825673453809665678-n

Bao la kwanza la Simba lilifungwa kipindi cha kwanza na Mzamiru Yassin dakika ya 38 akipokea pasi safi kutoka ya Okra bao ambalo lilidumu hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza.

Kipindi cha pili Simba waliingia na moto uleule waliouonyesha kipindi cha kwanza wakitumia dakika mbili tu kuandika bao la pili kupitia kwa Pape Sakho akipokea pasi safi kutoka kwa Phiri.

Bao hilo liliendelea kuamsha morali kwa wachezaji wa Simba ambao waliendelea kupeleka mashambulizi langoni mwa wapinzani wao.

simbasctanzania-313038318-925542725247036-6941443740718393852-n

Okra aliifungia Simba bao la tatu akipokea pasi safi kutoka kwa Tshabalala ambaye amehusika kwenye mabao mawili kwenye mchezo huo.

Mtibwa ililazimika kucheza pungufu wachezaji wawili Pascal Kitenge na Cassian Ponera baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu kitendo kilichochangia Simba kuutawala zaidi mchezo huo.

Dakika ya 42 beki wa Mtibwa Kitenge alionyeshwa kadi nyekundu baada ya kumchezea madhambi Sakho na dakika ya 67 Casian Ponera alitolewa nje baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano.

simbasctanzania-313211081-180777014538953-2515602992849300197-n

Kutoka kwa mabeki huyo kuliongeza ubora kwa Simba ambao waliendeleza kasi ya mashambulizi langoni mwa Mtibwa Sugar, timu zote zilifanya mabadiliko Mtibwa walimtoa Balama Mapinduzi, Baba Ubaya na nafasi zao zilichuliliwa na Omary Sultan na George Chota.

Wakati kwa upande wa Simba akitoka Phiri, Jonas Mkude, Tshabalala, Okra na Inonga nafasi zao zilichukuliwa na Gadiel Michael, Victor Akpan, Peter Banda, Kibu Denis na Mohammed Outtara.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top