Akifunga Mashindano ya Shirikisho la Wanasayansi Chipukizi Tanzania ambalo linahusisha wanafunzi wa Sekondari katika kufanya masuala ya utafiti wa kisayansi na ugunduzi wa teknolojia (Young Scientist Tanzania) Dr, Bora Haule ambaye ni kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Lindi amelipongeza shirika hilo kwa kuwa mstari wa mbele kuwawezesha wanafunzi na walimu kuwa wabunifu na wanasayansi wa siku zijazo
Dr, Bora Haule, kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Lindi akizungumza na wanafunzi washiriki mashindano ya Kisayansi yaliyofanyika mkoa wa Lindi. yakisimamiwa na shirika la Young Scientist Tanzania. |
Pia amewapongeza wanafunzi wote walioshiriki katika mashindano hayo na amesema kuwa wamechagua njia sahihi ya kuipenda Sayansi kwani uwepo wa Sayansi na teknolojia umerahisisha sana maiisha katika dunia ya leo.
“Uamuzi wenu wa kuwa wanasayansi chipukizi ni uamuzi sahihi ambao unafaida kwenu kwa nchi yetu na Dunia kwa ujumla. Tunatambua kupitia ninyi siku za mbele tutapata gunduzi na bunifu mbalimbali ambazo zinawezakuendelea kufanya dunia kuwa mahali salama Zaidi kwa kuishi.”
Dr. Bora amewataka ili kufikia malengo wanapaswa kuwasikiliza na kufuata maelekezo ya walimu wao , kujifunza Zaidi, kufanya majaribio na tafiti za kisayansi na kusoma gunduzi zilizofanyika ili waweze kuongeza maarifa.
Mashindano hayo yametoa washindi 6 ambao wataziwakilisha shule zao katika mashindano ya kitaifa ambayo yanatarajia kufanyika tarehe 8 Disemba, 2022 katika jiji la Dar es Salaam.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.