AZAM FC YAKATAA UTEJA KWA SIMBA SC YAICHAPA 1-0

Dakika Tisini za Dabi ya Mzizima zimemalizika hapa ndani ya Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa Azam Fc kukataa uteja kwa Simba Sc na kufanikiwa kupata ushindi wa goli 1-0.


Ni mtoto wa Mfalme Dube aliyepeleka kilio kwa wana lunyasi Simba kwa kufunga goli la kideo baada ya kumchungulia Aishi Manula na kumpimia mkwaju wa mbali uliomshinda na mpira kuzama kimiani mnamo dakika ya 35 ya kipindi cha kwanza.

Kwa Matokeo haya Simba inasalia nafasi ya tatu ikiwa imecheza michezo 7 ikikusanya alama 14, Azam wao wakikwea hadi nafasi ya 4 wakiwa wamecheza michezo 8 wakikusanya alama 14 huku kinara Yanga Sc akiwa kileleni kwa alama 17 akicheza michezo 7.

azamfcofficial-312729219-848879726545621-6859214447992458765-n azamfcofficial-312785034-656507836063979-9181780205160631518-n azamfcofficial-312972325-448610617259912-341571955325799166-n Soccer-Table-Graphic

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post