NIJUZE NIJUZE Author
Title: YOUNG SCIENTIST TANZANIA YAFUNGUA MASHINDANO YA KISAYANSI MKOA WA LINDI
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Shirikisho la Wanasayansi Chipukizi Tanzania (Young Scientist Tanzania) ambalo linahusisha wanafunzi wa Sekondari katika kufanya masuala ya ...

Shirikisho la Wanasayansi Chipukizi Tanzania (Young Scientist Tanzania) ambalo linahusisha wanafunzi wa Sekondari katika kufanya masuala ya utafiti wa kisayansi na ugunduzi wa teknolojia limefanya maonyesho ya kimkoa mkoani lindi ya kazi za sayansi na teknolojia, ambazo zimetengenezwa na wanasayansi chupikizi waliopo kwenye Shule mbalimbali za Sekondari mkoa wa Lindi.

Shule ishirini na tano ambapo wanafunzi jumla ya 50 na walimu 25 wameshiriki katika maonyesho hayo yaliyofanyika katika Shule ya Sekondani ya WAMA.

Dr. Gozbert Kamugisha akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Ufunguzi wa Mashindano ya Kisayansi yanayofanyika Shule ya Sekondari WAMA

 Akiongea na waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi wa maonyesho hayo  Dr, Gozbert Kamugisha ambaye ni mwanzilishi mwenza wa shirika la Young Scientist Tanzania amesema kuwa maonyesho hayo yatatoa washindi 6 ambao watashiriki mashindano ya kitaifa yatakayofanyika tarehe 8 Disemba, 2022 jijini Dar es Salaam.

Dr. Gozbert amesema mashindano hayo yatawasaidia wanafunzi hao kuweza kufanya kwa vitendo yale wanayofundishwa darasani katika masomo ya Chemistry, Biology na physics kutumia katika jamii ambapo itawaletea manufaa kwa kuboresha maisha yao ya kila siku.

“Tunaamin kwamba mwanafunzi anapofundishwa sayansi darasani na baadae akaifanya kwa vitendo kwa kuweza kuitafutia njia ya kuboresha maisha yake na jamii kwa ujumla sayansi ile anakuwa anaielewa vizuri Zaidi kuliko ile ambayo anafundishwa tu na kuishia pale darasani”.

Wanafunzi mbalimbali wa Shule za Sekondari Mkoa wa Lindi wakiwa tayari kwa mashindano ya Kisayansi yanayosimamiwa na Shirika la Young Scientist Tanzania

Amesema kuwa mashindano hayo kwa mkoa wa lindi ni mara ya Kwanza kufanyika lakini wanatarajia yataendelea kila mwaka kama ambavyo mikoa mingine ya Tanzania inafanya.

Akizungumzia faida ya maonyesho hayo mwalimu Sir Juma Ismail makota amesema kuwa Program hiyo ya Young Scientist Tanzania imewasaidia wanafunzi kwa kiasi kikubwa kutoka kwenye kukariri hadi kufanya kwa vitendo.

Mwalimu Juma Ismail Makota akiongea na waandishi wa habari baada ya ufunguzi wa Mashindano ya Kisayansi yanayofanyika Shule ya Sekondari WAMA

“Programu hii imesaidia wanafunzi wa kitanzania kwenye kuitransfomu sayansi kutoka kwenye kukariri hadi kufanya kwa vitendo kitendo ambacho kinawafanya wanafunzi kuipenda sayansi yenyewe”

Naye Muniri Hamisi Nakase ambaye ni mmoja wa wanafunzi shiriki katika mashindano hayo kutoka sekondari ya Ruangwa amesema kuwa program hiyo inawasaidia kutatua changamoto mbalimbali ambazo zinazoikabili jamii kiujumla

“Project yetu sisi inaenda kuwasaidi kwa kiasi kikubwa wakulima ambao walikuwa wanapoteza pesa nyingi kwa kununua mbolea za viwandani, sisi tumekuja na wazo la kutengeneza mbolea asilia kwa kutumia malighafi ambazo zinapatikana katika jamii yetu hii hii, hivyo watapunguza gharama na kupata mazao mengi.”

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top