DIAMOND PLATNUMZ, NAVY KENZO NA ALIKIBA WASHINDA TUZO ZA HIPIPO MUSIC AWARDS

HiPipo Music Awards
Wakali wa Bongo Fleva kutoka Tanzania Msanii Diamond Platnumz, Alikiba na Kundi la Navy Kenzo wameweza kutwaa Tuzo kupitia Tuzo za Hipipo Music ambazo zimetolewa Nchini Uganda katika Hoteli ya Serena Usiku wa Kuamkia February 5, 2017.

Diamond ameshinda Vipengele Viwili ambavyo ni Best 
East African video ambayo ni SALOME na Kipengele cha pili kilikuwa ni Quinquenial video Vanguard award, Hii Ni tuzo ya heshima ya Mtu alieanza muziki kipindi kisischopungua miaka mitano na kuweza kuvuka mipaka ya nchi yake nakuweza kuufikisha mziki wake mbali na kusaidia wengine. Tuzo hii kwa Tanzania anayo Diamond Pekee.

Alikiba ameweza kunyakua Tuzo ya Song of the year TZ
 kupitia wimbo wake wa Aje.

Huku Kundi la Navy Kenzo wakinyakua Tuzo kupitia kipengele cha Best East African act

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
KUWA KARIBU NASI LINDIYETU.COM
Usipitwe!! Ungana na Familia hii kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata Infortainment zote!! Usikose kujiunga na Youtube channel yetu ili kupata Exclusive mbalimbali kali kutoka LindiYetu TV

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post