Unknown Unknown Author
Title: TRENI ZA UMEME NA MAFUTA KUANZISHWA TANZANIA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli, amesema kuwa serikali imepanga kuondoa msongamano wa magari Jijini Dar es Salaam, iki...
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli, amesema kuwa serikali imepanga kuondoa msongamano wa magari Jijini Dar es Salaam, ikiwa ni pamoja mpango wa kuanzisha safari ya treni ya mafuta na umeme kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro.
Dkt. John Pombe Magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia mara baada ya kuendesha gari la Mwendo Kasi katika kituo Kikuu cha Mabasi yaendayo Haraka (BRT) mara baada ya kufungua rasmi Awamu ya Kwanza ya Miundombinu na Utoaji Huduma ya Mabasi yaendayo Haraka katika jiji la Dar es Salaam.

Rais Dk. Magufuli ametoa kauli hiyo leo Jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa awamu ya kwanza ya mradi wa miundombinu ya utoaji huduma kwa mradi huo wa BRT uliogharimu shilingi bilioni 403 ambapo amesema ujenzi huo utakuwa ni wa jumla ya kilometa 200 ambapo mchakato wa kumpata mkandarasi umeanza na kuwa awamu ya pili itakuwa ni njia ya treni inayoelekea katika mkoa wa Dodoma.

Hata hivyo Rais amewataka mawaziri wa ujenzi, Tamisemi na pamoja na uongozi wa DART kuwasilisha taarifa ya faida ya mradi huo kuanza ili kufahamu kama mradi huo unaendeshwa kwa faida au hasara.
Dkt. John Pombe Magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipita kwenye mashine hizo mara baada ya uzinduzi wa Awamu ya Kwanza ya Miundombinu na Utoaji Huduma ya Mabasi yaendayo Haraka katika jiji la Dar es Salaam.

"Mawaziri mmetoa taarifa nzuri sana hapa lakini mmeninyima raha kwa kutonipa taarifa ya pesa za faida zilizopatikana kutokana na mradi huu" alisema Rais Magufuli

Amesema alitaka kujua kama zipo fedha za faida za mradi huo ili atoe maagizo kuhusu eneo la Kimara kujengwa kituo kingine kikubwa sehemu ya kuegesha magari ili wenye magari binafsi waegeshe na kupata magari ya mwendo wa haraka.


++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
KUWA KARIBU NASI LINDIYETU.COM
Usipitwe!! Ungana na Familia hii kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata Infortainment zote!! Usikose kujiunga na Youtube channel yetu ili kupata Exclusive mbalimbali kali kutoka LindiYetu TV

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top