THOMAS ULIMWENGU RASMI KUKIPIGA BARANI ULAYA

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Emmanuel Ulimwengu anaondoka nchini leo kwenda kukamilisha usajili wake klabu ya AFC Eskilstuna ya Ligi Kuu ya Sweden.
Thomas Emmanuel Ulimwengu
Akizungumza hii leo, Ulimwengu amesema kwamba baada ya mazungumzo ya awali na klabu hiyo anakwenda kusaini mkataba wa miaka miwili na klabu hiyo, ambayo awali ilikuwa inajulikana kama FC Cafe Opera na Vasby United.

“Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa watu wangu wote wa karibu kama Jamal Kisongo ambao wamekuwa karibu na mimi kwa kipindi chote hiki na kunipa ushauri hadi kufikia maamuzi haya ya kujiunga na timu hii. Tumekataa ofa nyingi sana na kuikubali hii kwa sababu za msingi sana,” alisema.

Kwa upande wa meneja wake, Jama Kisongo, amesema masuala ya mkataba wa mchezaji huyo bado hayajakamilika, na kwamba akifika takamilisha kila kitu.

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
KUWA KARIBU NASI LINDIYETU.COM
Usipitwe!! Ungana na Familia hii kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata Infortainment zote!! Usikose kujiunga na Youtube channel yetu ili kupata Exclusive mbalimbali kali kutoka LindiYetu TV

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post