Na. Ahmad Mmow. Nachingwea
Sakata la kuchelewa kwa malipo ya wakulima wakorosho limechukua sura mpya. Baada ya mbunge wa jimbo la Nachingwea mkoani Lindi, Hassan Masala kukiandikia barua chama kikuu cha RUNALl, kuomba ufafanuzi wa mwenendo wa ununuzi wa zao hilo na changamoto zilizo jitokeza.
Katika barua yake ya tarehe 3 mwezi huu, ambayo amekiri kuwa aliandika. Mbunge huyo anayetokana na Chama Cha Mapinduzi amekiomba chama hicho kimpe ufafanuzi na maelezo sahihi ya sababu ya changamoto zilozojitokeza katika kipindi chote cha msimu wa 2016/2017.
Lengo likiwa nikujielekeza kwenye tathimini, ili kuwa na kumbukumbu sahihi ambazo kwa nafasi yake ya ubunge zitasaidia kujipanga kwa ajili ya kuboresha mfumo uliopo katika msimu ujao wa 2017/2018.
Mbunge huyo ambae ni kati ya wabunge wanne waliopitia CCM kati ya majimbo nane ya uchaguzi yaliyopo katika mkoa huu wa Lindi, miongoni mwa hoja ambazo amezichukua kama changamoto zinazihitaji majibu kutoka kwenye chama hicho ni pamoja na kutaka kujua nisababu zipi zilizosababisha wakulima kuchelewa kulipwa.
Ikiwamo waliouza korosho tangu mwezi oktoba mwaka jana, lakini hadi sasa hawajalipwa, sababu za kampuni zilizoshinda zabuni kushindwa kulipa fedha za wakulima ndani ya siku sita kama zilivyotakiwa na hatua gani zimechukuliwa na chama hicho dhidi ya kampuni hizo.
Masala pia amehoji ni kiasi gani cha magunia chakavu waliuziwa wakulima na kuingizwa kwenye mzunguko. Ikizingatiwa kwamba magunia ni miongoni mwa vifaa ambavyo gharama zake zinakatwa kutoka kwenye mjengeko wa bei. Tena kwa magunia mapya nasio chakavu.
"Niutaratibu gani umetumika kukata fedha za wakulima kwa magunia hayo chakavu kwa kuzingatia kwamba fedha zilizopo kwenye mjengeko wa bei ni za magunia mapya, makadirio ya makato hayo yamezingatia vigezo gani," amehoji Masala.
Mbunge huyo ameendelea kusema baadhi ya vyama vya msingi vya ushiririka (AMCOS) wilayani humo vimeshindwa kufanya malipo kwa wakulima kwa wakati kwasababu ya kusahaulika na kuchanganywa kwa stakabadhi za maghalani (wherehouse) na kusababisha wakulima wengi kuuza korosho zao kwenye minada iliyokuwa na bei ndogo wakati walipeleka mwanzoni mwa misimu na minada ya awali ambayo ilikuwa na bei kubwa.
Hivyo Masala amekiomba chama hicho kumpa maelezo ya kina ya sababu za usahalifu na uchanganyaji huo ambao ulikuwa unaripotiwa na vyama vya msingi.
"Aidha kwa mkanganyiko huo naomba kufahamishwa utaratibu uliotumika kukokotoa malipo ya wakulima waliouza korosho kwenye minada yenye bei za juu, lakini kutokana na usahaulifu huo korosho zao zimepelekwa kwenye minada ya bei ndogo. Kama ofisi kupitia idadi ya korosho ambazo hazikuuzwa kwa wakati naomba kupata makadirio ya takwimu ya kiasi cha fedha ambazo wakulima wamepoteza kwasababu ya kuuza kwenye minada iliyokuwa na bei ndogo," aliongeza kuhoji Masala.
Aidha mbunge huyo ameikumbusha kamati ya muda chama hicho kwamba miongoni mwa majukumu yake ni kusimamia usajili wa chama hicho ambacho bado hakijasajiliwa na hatimae kifanye uchaguzi utakaosababisha kupanga safu itayokamilika kiutendaji itakayoweza kupunguza baadhi ya changamoto na kuongeza ufanisi katika msimu ujao.
Mwenyekiti wa kamati ya muda wa RUNALI, Abdulaziz Liega alikiri kufikishwa kwenye ofisi kuu ya chama hicho barua hiyo ambayo alipelekewa meneja wa chama hicho.
Hata hivyo alihaidi kumpa majibu mbunge huyo kipindi kifupi kijacho.
"Nikweli barua hiyo tumeipata natunajipanga kumjibu, ingawa baadhi ya hoja zimeshafanyiwa kazi kama ya makapuni kuchelewa kulipa, tayari kampuni zote zimeshalipa na wakulima wanaendelea kulipwa. Kwahiyo sidhani kama hoja hiyo inataka majibu, ila tutamjibu kama alivyoomba," alisema Liega.
Wakati hali ikiwa hivyo bado baadhi ya wakulima wa kata ya Matekwe tarafa ya Kilimarondo katika wilaya hiyo ya Nachingwea, ambao korosho zao walipeleka katika chama cha msingi cha ushirika cha Mbondo (Mbondo AMCOS) wameendelea kugomea kulipwa kwa bei ya shilingi 2500 kwa kila kilo moja. Kwa madai ya kutoridhishwa na mchakato wa ununuzi wa korosho zao.
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
KUWA KARIBU NASI LINDIYETU.COM
Usipitwe!! Ungana na Familia hii kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata Infortainment zote!! Usikose kujiunga na Youtube channel yetu ili kupata Exclusive mbalimbali kali kutoka LindiYetu TV
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.