Unknown Unknown Author
Title: MSD YASEMA UPATIKANAJI WA DAWA NCHINI UMEIMARIKA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mkurugenzi wa Bohari ya Dawa (MSD) Laurean Bwanakunu (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akitoa taar...
Mkurugenzi wa Bohari ya Dawa (MSD)
Mkurugenzi wa Bohari ya Dawa (MSD) Laurean Bwanakunu (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akitoa taarifa ya kuimarika kwa upatikanaji wa dawa nchini. Kulia ni Ofisa Mwandamizi wa Idara Habari Maelezo, Zamaradi Kawawa.

Na Dotto Mwaibale
MKURUGENZI wa Bohari ya Dawa (MSD) Laurean Bwanakunu amesema hali ya upatikanaji wa dawa kwa sasa imeboreshwa kutoka asilimia 54 iliyokuwepo mwaka jana, hadi kufikia asilimia 74 hivi sasa.

Ameuhakikishia umma kuwa upatikanaji wa dawa utaimarika mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu hadi kufikia asilimia 90.

Amesema kwa sasa kati ya aina za dawa muhimu 135 zinazohitajika kuwepo MSD dawa aina 100 zinapatika kwenye maghala ya MSD.

Mkurugenzi wa MSD, Bwanakunu ameyasema hayo mbele ya waandishi wa habari, Dar es Salaam leo Ukumbi wa Idara ya habari Maelezo, alipokuwa kwenye mkutano ulioandaliwa na idara katika jukumu lake la kutoa nafasi kwa Idara na Taasisi za serikali kuelezea utekelezaji wa majukumu yao.

Katika hatua nyingine, Bwanakunu ameeleza kuwa, MSD imefanikiwa kurejesha Maghala iliyokuwa imekodi kwa ajili ya kuhifadhia vifaa tiba, hatua ambayo inaokoa sh.Bilioni 4 ambazo zilikuwa zikilipwa kama kodi kila mwaka.

Ameongeza kuwa, tayari wamekabidhiwa kiwanja eneo la Luguruni, wilayani Ubungo walichopewa na Rais John Magufuli ambacho kitatumika kujenga ofisi za Kanda ya Dar es Salaam.

Kuhusu maduka, ameeleza kuwa wiki ijayo wanatarajia kuzindua duka la dawa la MSD mkoani Katavi, ambalo litaifanya MSD kuwa na jumla ya maduka Saba, mengine yakiwa mkoani Arusha, Dar es Salaam, Mwanza, Lindi, Geita na Mbeya.

Akijibu swali juu ya ukosefu wa vifaa vya kujifungulia wajawazito Mkurugenzi Mkuu amesema vipo vyakutosha, na zabuni ya manunuzi ya vifungashio kwa ajili ya vifaa hivyo vya kujifungulia viko katika mchakato wa kumpata mshitiri.

Ameeleza kuwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu anaangalia namna ya kuwawezesha akina mama wasio kuwa na uwezo wakununua vifaa hivyo ambapo utaratibu huo atautoa baadae.

Kwa sasa MSD inanunua dawa na vifaa tiba moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji, ilikuhakikisha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba unakuwa endelevu na kupunguza gharama za ununuzi wa dawa hizo, ambazo asilimia 80 zinatoka nje ya nchi.

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
KUWA KARIBU NASI LINDIYETU.COM
Usipitwe!! Ungana na Familia hii kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata Infortainment zote!! Usikose kujiunga na Youtube channel yetu ili kupata Exclusive mbalimbali kali kutoka LindiYetu TV

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top