Unknown Unknown Author
Title: MKUU WA MKOA WA LINDI APIGA MARUFUKU SHUGHULI ZOTE ZA KIMILA, SABABU HII HAPA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi amepiga marufuku kufanyika kwa shughuli zozote zile za kimila zinazotumia chakula kuanzia mwezi ...
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi amepiga marufuku kufanyika kwa shughuli zozote zile za kimila zinazotumia chakula kuanzia mwezi wa huu wa Disemba mpaka Mei 2017.
Mhe. Godfrey Zambi
Shughuli hizo ni pamoja na Unyago, Ndoa na Ngoma za Majini. Alisema shughuli hizo zinazofanywa na Wananchi zimekuwa zinatumia chakula kingi hali hii inaweza kupelekea kutokea kwa janga la njaa mkoani hapo.

Mkuu huyo wa Mkoa wa Lindi aliwataka Wananchi kuwa wavumilivu na waelewa kwani janga la njaa halichagui Mkoa bali matumizi mabovu ya chakula yanaweza kuleta janga hilo kwa Wananchi wote.

"Sitaki kuwa Mkuu wa Mkoa ambaye Mkoa wangu umekutwa na janga la njaa kwani hii ni aibu kubwa hivyo Watu wawe makini katika matumizi ya chakula hata kama chakula wanalima kwa nguvu zao wenyewe".
Chanzo: Cloudsfm
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
KUWA KARIBU NASI LINDIYETU.COM
Usipitwe!! Ungana na Familia hii kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata Infortainment zote!! Usikose kujiunga na Youtube channel yetu ili kupata Exclusive mbalimbali kali kutoka LindiYetu TV

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top