Hivi karibuni zimesambaa picha kwenye mitandao ya kijamii zikimuonyesha msanii wa Bongofleva Rashid Makwilo ‘Chid Benz’ akionekana kurudi kwenye dawa za kulevya.
December 31 2016 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amekutana na kufanya mazungumzo na mama wa Chid Benz, baada ya kuonana na mama yake Chid Benz haya ni maneno aliyoyaandika kwenye ukurasa wake wa Instagram……..
Nimekutana na kufanya mazungumzo na mama wa msanii Rashid Makwilo “Chid Benz” ambaye kwasasa amepatwa na tatizo la Dawa za kulevya. Inasikitisha na haivumiliki kuona nguvu kazi ya Taifa inapotea huku wauzaji wakinufaika kwa pesa haramu.
Ifahamike wazi vita ya serikali dhidi ya magenge, wauzaji na wasambazaji wa madawa ya kulevya imeongezeka hasa katika awamu hii ya tano chini ya Mh.Rais J.P.Magufuli,hivyo anayejihusisha kwa namna yoyote ni vema akaamua kuachana nayo kabla hajakutwa na mkono wa dola.
Mbali ya vyanzo vya taarifa tulivyonavyo, ni wajibu wa kila aliye RAIA MWEMA kutoa taarifa zitakazo saidia kuangamiza biashara haramu ya madawa ya kulevya. Naishukuru familia ya Chid Benz kwa jitihada wanazozifanya kuhakikisha kijana mwenzetu anarejea katika hali yake ya kawaida. Unaweza kuimba,unaweza kufanikiwa, unaweza kutatua matatizo yako bila kutumia madawa ya kulevya.
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
KUWA KARIBU NASI LINDIYETU.COM
Usipitwe!! Ungana na Familia hii kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata Infortainment zote!! Usikose kujiunga na Youtube channel yetu ili kupata Exclusive mbalimbali kali kutoka LindiYetu TV
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.