DARASSA ATANGAZA MIUJIZA ZAIDI MWAKA 2017

Mwaka 2016 ni mwaka wa historia kwa Darassa rapa ambaye amejipatia umaarufu zaidi na kufanya show nyingi huku akishuhudia mambo makubwa zaidi katika muziki wake toka alipoanza kufanya muziki.
Darassa
Darassa mwenyewe anakiri wazi kuwa mwaka 2016 kwake ulikuwa mwaka wa miujiza kwa jinsi ambavyo ameweza kuja na kubadili upepo wa muziki wa Tanzania na kuingia katika akili za watanzania walio wengi kutokana na kazi yake ya 'Muziki' ambayo imefanya mengi makubwa ndani ya muda mfupi sana.

Katika ukurasa wake wa Instagram rapa Darassa aliandika ujumbe ambao unasomeka "2017 miujiza inaendelea" huku baadhi ya mashabiki wake wakitafsiri kuwa rapa huyo ataendelea kufanya vyema na kufanya kazi ambazo huenda zikawashangaza tena kama ilivyokuwa kwa ngoma yake ya "Muziki".

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
KUWA KARIBU NASI LINDIYETU.COM
Usipitwe!! Ungana na Familia hii kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata Infortainment zote!! Usikose kujiunga na Youtube channel yetu ili kupata Exclusive mbalimbali kali kutoka LindiYetu TV

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post