BAO la kwanza kwa Mchezaji Bora wa Bundesliga ya huko Germany Msimu uliopita katika EPL, Ligi Kuu England, Henrikh Mkhitaryan, Leo limewapa Manchester United ushindi wa 1-0 dhidi ya Tottenham Hotspur Uwanjani Old Trafford.
Bao hilo lilipatikana Dakika ya 29 kufuatia Pasi safi ya Ander Herrera kunaswa na Mkhitaryan na kuachia Shuti lililotinga Wavuni.
Paul Pogba angeweza kuipatia Man United Bao la Pili lakini Frikiki yake iligonga Posti lakini Bao hilo pekee la Mkhitaryan limetosha kuipa Man United ushindi wake wa kwanza katika Mechi 3 za EPL ambazo walitoka Sare 1-1 na Arsenal, West Ham na Everton, Mechi ambazo zote walitawala na kustahili ushindi.
Hata hivyo, Mechi hii iliisha vibaya kwa Man United na Mkhitaryan baada kuumizwa na Rose wa Spurs Rafu ambayo Man United walidai ni Penati.
Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Armenia alitolewa Uwanjani kwa Machela.
Ushindi huu wa Man United umeikita Nafasi ya 6 wakiwa Pointi 3 nyuma ya Timu ya 5 Spurs na 6 nyuma ya Timu ya 4 Man City.
VIKOSI: Manchester United (4-3-3): De Gea, Valencia, Jones, Rojo, Darmian, Ander Herrera (Fellaini 90+5), Carrick, Pogba, Mkhitaryan (Bailly 84), Ibrahimovic, Martial (Rashford 72,).
Akiba: Mata, Rooney, Blind, Romero.
Kadi: Valencia, Pogba, Mkhitaryan
Goli: Mkhitaryan 29
Tottenham Hotspur (4-2-3-1): Lloris, Walker, Alderweireld, Vertonghen, Rose, Wanyama, Dembele (Winks 67), Eriksen (Nkoudou 82), Alli, Son (Sissoko 57,), Kane.
Akiba: Vorm, Dier, Wimmer, Davies.
Kadi: Wanyama, Walker
Refa: Robert Madley (West Yorkshire)
Matokeo: Jumapili Desemba 11
Chelsea 1 - 0 West Bromwich Albion
Manchester United 1 - 0 Tottenham Hotspur
Southampton 1 - 0 Middlesbrough
Liverpool 2 - 2 West Ham United
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.