Na Mwandishi wetu
Wanafunzi wenye vipaji katika mchezo wa soka, riadha, na mpira wa kikapu, wanatarajiwa kuwasili Jumamosi katika shule ya Sekondari ya Lord Barden Memorial iliyopo Bagamoyo, Mkoani Pwani tayari kwa majaribio ya kupata udhamini wa masomo shuleni hapo.

Kijana Andrew Elliot Hamisi ni mmoja wa wanafunzi aliyeitwa kwenye majaribio hayo kutoka Shule ya Msingi Mailisita iliyopo wilayani Masasi.
Akizungumza na Lindiyetu.com, Mratibu wa mpango huo, Michael Maurus, alisema kuwa Wanafunzi walioomba nafasi hiyo kupitia fomu zilizotolewa kwenye magazeti ya BINGWA na DIMBA, wanatakiwa kuwasili ofisi za New Habari (2006) Limited zilizopo Sinza Kijiweni, Dar es Salaam, Jumamosi ya Desemba 31, kuanzia saa 10:00 - 11:00 jioni tayari kwa safari ya Lord Barden.
Alisema kuwa wanafunzi hao watakaa shuleni hapo kwa siku tatu, wakinolewa na kushindanishwa ili kupata wale wenye vipaji vya hali ya juu ambao watapata udhamini wa masomo kwa ufadhili wa Mkurugenzi wa Lord Barden Sekondari, Kanali Mstaafu, Iddi Kipingu, pamoja na wadau wengineo.
Alisema kuwa wamewaalika makocha wa timu za vijana wa Yanga, Simba na Timu ya Taifa pamoja na wadau wengineo ili waweze kuwachagua vijana ambao mwisho wa siku watawasomesha na kuwaendeleza kimichezo na klabu zao.

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
KUWA KARIBU NASI LINDIYETU.COM
Usipitwe!! Ungana na Familia hii kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata Infortainment zote!! Usikose kujiunga na Youtube channel yetu ili kupata Exclusive mbalimbali kali kutoka LindiYetu TV
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.