Unknown Unknown Author
Title: RC ZAMBI KUWACHONGEA KWA RAIS WASIO PELEKA FEDHA ZA VIKUNDI VYA WANAWAKE NA VIJANA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na. Ahmad Mmow, Nachingwea. BAADA ya kubaini baadhi ya halmashauri zilizopo katika mkoa Lindi, kusuasua kupeleka 10% ya fedha zinazotoka...
Na. Ahmad Mmow, Nachingwea.
BAADA ya kubaini baadhi ya halmashauri zilizopo katika mkoa Lindi, kusuasua kupeleka 10% ya fedha zinazotokana na mapato yake ya ndani kwa vikundi vya wanawake na vijana.
Godfrey Zambi
Mkuu wa mkoa huu, Godfrey Zambi, amesema atawachongea kwa Rais wakurugenzi watendaji na wakuu wa wilaya ambao halmashauri zao hazipeleki fedha hizo kwa wakati kwa vikundi vya wanawake na vijana.

Zambi ametoa tishio hilo leo mjini Nachingwea, alipozungumza na baadhi ya watumishi, madiwani, wenyeviti wa serikali za vijiji, maofisa tarafa, watendaji wa kata na vijiji na viongozi wa chama kikuu cha ushirika cha RUNALI.

Zambi alisema kupeleka 10% ya fedha zinazotokana na mapato yake ya ndani kwa vikundi vya vijana na wanawake sio suala la hiari, bali ni lazima.

Kwakutambua ukweli huo, amesema hatakuwa na muda wakuwabembeleza wanashindwa kutekelezo agizo hilo halali la serikali.

Kwahiyo hatakuwa na njia nyingine zaidi ya kuwachongea kwa Rais ambae amewateua ili awachulie hatua kwa kupuuza maagizo yake.

Amebainisha kwamba baadhi ya wakurugenzi watendaji wa halmashauri hawapeleki fedha hizo kwa wakati na wengine wanapelekea kiasi kidogo tofauti na inavyotakiwa.

Aidha mkuu huyo wa mkoa amewataka wakuu wa wilaya, wakurugenzi watendaji na wakuu wa idara wahakikishe watumishi wanatimiza wajibu wao.

Ikiwamo kuheshimu rasilimali muda kwa kutotumia vibaya muda wa kazi."Kila mtumishi awe na ratiba na mpango kazi, simu zenu mnazitumia vibaya, simu zenyewe nyingi hazitumiki kwa mambo ya msingi bali ya ovyo," alisema Zambi.

Mkuu huyo ambae pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa, pia aliwaka baadhi watumishi wa umma wenye tabia ya kuwadharahu watumishi wenzao kwa sababu ya vyeo vyao kuacha tabia hiyo.

Akibainisha kuwa tabia hiyo inakwamisha utendaji wa kazi katika maeneo mengi ya taasisi na idara za umama. Wakati watumishi wote nisawa na wanahaki ya kuheshimiwa.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top