Unknown Unknown Author
Title: BODI YA KOROSHO YAMPONGEZA NA KUMSHUKURU RC ZAMBI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na. Ahmad Mmow, Lindi. Bodi ya korosho imempongeza na kumshukuru mkuu wa mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi kuruhusu wafanyabiashara kusafiris...
Na. Ahmad Mmow, Lindi.
Bodi ya korosho imempongeza na kumshukuru mkuu wa mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi kuruhusu wafanyabiashara kusafirisha korosho kwa njia ya barabara badala ya maji.
Godfrey Zambi
Pongezi na shukrani hizo zilitolewa hivi karibuni na mkaguzi mwandamizi wa ndani wa bodi hiyo, Christopher Mwaya, alipozungumza wakati wa ufunguzi wa zabuni katika mnada wa saba wa korosho unaoratibiwa na chama kikuu cha ushirika cha Lindi Mwambao, uliofanyika manispaa ya Lindi.

Akizungumza kwenye mnada huo ambao ulikuwa na kampuni nane zilizoomba kununua zao hilo linalozalishwa kwa wingi katika mikoa ya Lindi na Mtwara. Mwaya alisema uamuzi wa mkuu huyo wa mkoa, ambae alikuwepo kwenye mnada huo, niwakupongezwa na kushukuriwa. Kwasababu njia ya awali ilianza kuathiri ununuzi wa zao hilo katika mikoa ya Lindi na Mtwara.

Alisema kutokana na bandari ya Mtwara kuzidiwa na mizigo, wanunuzi walisita kuendelea kununua kutokana na kukosa maghala ya kuhifadhia. Alisema hali hiyo ilisababisha korosho kushindwa kununuliwa kwa be mzuri kutokana na kujitokeza kampuni chache katika kwenye minada iliyofanyika hivi karibuni.
"Nidhahiri kutojitokeza waombaji wengi kwenye minada kulisababisha kukosekana ushindani,hivyo hata bei zilishuka," alisema.

Mwaya alisema uamuzi huo utarejesha ushindani na kupandisha bei ya zao hilo katika minada ijayo. Kwa upande wake mkuu wa mkoa aliiongeza kusema licha ya bandari hiyo kuelemewa na mzigo lakini pia kuna uhaba mkubwa wa vifungashio mjini humo.

Hali ambayo ilikuwa inawa athiri katika usafirishaji wa zao hilo. Hivyo kusababisha korosho kutonunuliwa na wafanya biashara.
"Kwania njema na kwamaslahi ya wakulima wa mkoa huu,tuliamua korosho zilizonunuliwa katika mkoa huu na kukwama kwenye maghalani kule Mtwara zisafirishwe kwa njia ya barabara," alisema Zambi.

Mkuu huyo wa mkoa, alisema serikali ya mkoa ilifikia uamuzi huo na kutengua uamuzi wa awali baada ya kubaini bandari ya Mtwara ilishaelemewa na mizigo.

Hali ambayo ingeishia usumbufu kwa wanunuzi na hata wasimamizi na waratibu wa zao hilo. Ikiwamo bodi ya korosho.

Kwa mujibu wa meneja wa chama kikuu cha Lindi Mwamba, Hassan Vudu, Katika mnada huo kampuni nane zilijitokeza kuomba kununua korosho kilo 954,000 zilizopo katika maghala ya BUCO (Lindi) na Lindifarmers (Mtama).

Kampuni zilizoteuliwa kununua katika maghala ya BUCO ni Export Trading kilo 20,000 kwa bei ya shilingi 3,035/= kwa kila kilomoja na Saweya kilo 254,000 kwa bei ya shilingi 3,034/=. Ambapo katika maghala ya Lindi farmers kampuni zilizoteuliwa ni DPS, kilo 100,000 kwa bei ya shilingi 3,252/=, Export Trading kilo 300,000 kwa bei ya shilingi 3,035/= na Saweya kilo 100,000 kwabei ya shilingi 3,034/=.
**********

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top