WANANCHI WATAKIWA KUPUNGUZA LAWAMA KWA MADAKTARI.

Na. Ahmed Mmow. Lindi
WANANCHI wametakiwa kutambua na kuthamini kazi zinayofanywa na madaktari na waganga badala ya kuwalaumu bila sababu za msingi.
Kassim Majaliwa
Hayo yamesemwa leo mjini Ruangwa, na waziri kuu, Kassim Majaliwa baada ya kupokea msaada wa bati 100 zenye thamani ya takribani shilingi milioni 2, kutoka kwa mbunge wa viti maalum wa mkoa wa Lindi, Amida Mohamed Abdallah.

Waziri mkuu Majaliwa amesema wananchi hawanabudi kuthamini na kutambua kazi kubwa na ngumu inayofanywa na wataalamu hao wa afya badala ya kuwalaumu na kuwapunguzia ari ya kufanya kazi.

Amesema idadi ya watalaamu hao ni ndogo na serikali inatambua hilo. Hata hivyo wanajitahidi kufanya kazi kwa juhudi kubwa. Hivyo wananchi wawape ushirikiano.

Amesema katika kipindi cha miaka mitano, serikali itahakikisha sekta ya afya na huduma za matibabu zinaboreka. Ikiwamo ujenzi wa zahanati katika kila kijiji. 

Kwa upande wake, mbunge Amida, alisema bati hizo alizotoa ili zitumike kwa ujenzi wa wodi ya akinamama ni utekelezaji wa ahadi aliyotoa kwa waziri mkuu huyo mwezi Aprili mwaka huu.
"Nilihaidi kuchangia bati ili zitumike kwa ujenzi wa wodi ya akina mama,kwasababu naunga mkono juhudi za serikali za kuboresha huduma za afya," alisema Amida.

Waziri Majaliwa amehitimisha leo ziara yake ya siku nne katika mkoa huu wa Lindi.
***********

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post