Unknown Unknown Author
Title: VIONGOZI JARIBU AMCOS WATAKIWA WAELEZE WALIKOPELEKA FEDHA ZA WAKULIMA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na.Ahmad Mmow, Lindi. UNUNUZI wa korosho kutoka kwa wakulima katika msimu wa 2016/2017,ukiwa umeanza rasimi. Mkuu wa wilaya ya Kilwa mkoan...
Na.Ahmad Mmow, Lindi.
UNUNUZI wa korosho kutoka kwa wakulima katika msimu wa 2016/2017,ukiwa umeanza rasimi. Mkuu wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi, Christopher Ngubiagai amewataka viongozi na watendaji wa chama cha msingi cha ushirika JARIBU waeleze sababu za kutowalipa wakulima waliouza zao hilo kwenye chama hicho msimu uliopita.
korosho
Ngubiagai aliyetoa agizo hilo katika kijiji cha Kitumbi Nkunya kata ya Mingumbi, mwanzoni mwa wiki hii baada ya wakulima wa zao hilo kumueleza hawajalipwa takribani shilingi 5.00 milioni. Ikiwa nimalipo ya msimu uliopita. 

Alisema baadhi ya viongozi na watendaji wa vyama vya msingi vya ushirika(AMCOS) wamekuwa chanzo cha wananchi kuuchukia mfumo wa malipo ya stakabadhi ghalani kutokana na kukosa uaminifu.

Hivyo viongozi na watendaji wa chama hicho wampelekee maelezo sahihi ya sababu zinazosababisha wakulima hao kutolipwa.
"Nataka ndani ya siku 14 mnipe maelezo,sipotayari kuona wakulima wanahamasishwa wazalishe korosho kwa wingi wakati viongozi na watendaji wanawadhulumu,"alisema Ngubiagai.

Mkuu huyo wa wilaya ambae yupo kwenye ziara ya kuwahamasisha wakulima wafungue akaunti za benki ili malipo ya mazao yao, ikiwamo korosho yalipwe kupitia kwenye akaunti hizo.

Alisema iwapo hataridhirishwa na maelezo ya viongozi hao ataliagiza jeshi la polisi wilayani humo liwakamate na kuwafungulia shitaka la wizi.

Aidha alitoa wito kwa wakulima kuupokea mfumo wa malipo kwa njia ya benki kwa sababu utawahakikishia usalama wa fedha zao na wenyewe.

Alibainisha kuwa nia ya serikali ni njema, kwani mfumo wa malipo uliopo, unahatarisha pia usalama wa wasafirishaji wa fedha wanaopeleka kwenye vyama vya msingi.
"Fedha nyingi zimeporwa na majambazi wakati zinasafirishwa, nakusababisha wakulima kutolipwa hadi sasa," alisema.

Awali kupitia mkutano huo wa hadhara, wakulima hao walimueleza mkuu huyo wa wilaya wanakatishwa tamaa ya kuzalisha korosho. Kwamadai wanaonufaika na zao hilo ni viongozi na watendaji wa vyama msingi badala ya wakulima wenyewe. 
Kwamadai kwamba wanadhulumiwa na hakuna hatua zozote za kisheria zinazochukuliwa dhidi ya viongozi na watendaji wanaowadhulumu.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top