Kufuatia habari mbalimbali zilizokuwa zimesambaa kumuhusu Mfalme wa Rhymes na mwanachama wa Chama cha ACT Wazalendo Selemani Msindi maarufu kama Afande Sele kuwa amekihama chama hicho.

Habari hizo zilizidi kudhihiri zaidi kufuatia ziara ya Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan katika Mkoa wa Morogoro ambapo Afande Sele alipata fursa ya kuzungumza na wananchi jambo ambalo liliwashtua wengi na kudhani amekiama chama hicho rasmi.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram msanii huyo amekanusha tetesi hizo na kusema hazina ukweli wowote, huku akieleza kuwa sio vibaya yeye kuitikia wito wa Makamu wa Rais ambaye ni kiongozi wake wa Serikali na kuwataka wanaopotosha watu waacha kusambaza taarifa hizo.

“Aisee Watanzania sisi wengi wetu hata sijui nani katuloga kiasi cha kufunga kabisa uwezo wetu wa kufikiri nakushindwa kutofautisha hata vitu vidogo na vya kawaida sana vinavyotokea ktk maisha yetu ya kila siku hebu tazama hiyo picha utaona mimi nipo na Makamu wa Rais, Mkuu wa Mkoa wetu na viongozi wengine wa Serikali, hiyo inamaanisha kwamba hapo niliitikia wito wa serekali sio wito wa chama chochote cha siasa” Hayo ni baadhi ya maneno aliyoandika Afande Sele kwenye ukurasa wake wa Instagram.
***************
Tags
HABARI ZA KITAIFA