STUDIO YA WASAFI RECORDS YAENDELEA KUBORESHWA, SASA KULETWA KIFAA HICHI KIPYA

Mkali wa wimbo ‘Salome’ Diamond Platnumz amesema ameagiza mixer kubwa nje ya nchi ili kuboresha studio ya ‘Wasafi Records’ ambayo tayari imeshaanza kufanya hits kadhaa ambazo zinafanya vizuri katika chart mbalimbali za muziki nchini.
Diamond Platnumz
Muimbaji huyo wiki hii alitembelewa ofisini kwake na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira, January Makamba na kumueleza mambo mbalimbali ambayo atayafanya ili kuboresha ofisi hiyo.

“Kwa sasa tunasubiri mixer ifike kwa sababu tuliambiwa hatuwezi kuichukua dukani mpaka tutoe order waitengeneze,” Diamond alimwambia Waziri January. “Zingekuwa ni zile ndogo ndogo wangenipa lakini kwa sababu hii ni kubwa sana lazima utoe order, na tayari nimeshalipia kama dola 20,000 na kitu,”

Pia Waziri January Makamba alimsifia producer wa ‘Wasafi Record’ Lizer kwa kufanya maajabu kwenye wimbo mpya wa Diamond ‘Salome’ ambao kwa sasa unafanya vizuri.

****************

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post