Yanga ndio waliotangulia kufunga Bao katika Dakika ya 26 kupitia Amisi Tambwe aliekontroli Mpira wa Pasi ndefu ya Mbuyu Twite na kugeuka haraka na kumchambua kama karanga Kipa wa Simba Vincent Angban.
Bao hilo lilizua hasira kwa Wachezaji na Mashabiki wa Simba wakidai Tambwe alicheza Mpira kwa Mkono na rabsha zikamfanya Kepteni wa Simba Jonas Mkude ale Kadi Nyekundu toka kwa Refa Martin Saanya.
Jukwaani, Mashabiki wa Simba wakaheuka na kuleta vurugu na kuvunja Viti na Gemu kusimama kwa Dakika kadhaa Polisi wakiingilia kati.
Hadi Mapumziko Yanga 1 Simba 0.
Kipindi cha Pili, Yanga wakionekana kuridhika na Bao lao, Simba walijipanga upya na hatimaye kusawazisha Dakika ya 87 kwa Kona iliyopigwa na Shiza Kichuya na moja kwa moja kutinga wavuni huku Kipa Ali Mustapha ‘Barthez’ akipungia hewa na kumuiga Barthez mwenzake wa Man United kutoa ‘maboko’ katika Mechi muhimu.
Matokeo haya yanaendelea kuwafanya Simba wakae kileleni wakiwa na Pointi 17 kwa Mechi 7 na Yanga kubaki wa 3 wakiwa na Pointi 11 kwa Mechi 6.
Timu ya Pili ni Stand United wenye Pointi 12 kwa Mechi 6 wakifuata Azam FC na Mtibwa Sugar wote wakiwa na Pointi 10 kila mmoja na wamecheza Mechi 6 kila mmoja.
VIKOSI: YANGA: Ali Mustapha, Juma Abdul, Haji Mwinyi, Vicent Bossou, Kelvin Yondani [Andrew Vincent], Mbuyu Twite, Juma Mahadhi [Simon Msuva], Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe, Donald Ngoma, Deus Kaseke [Haruna Niyonzima]
Akiba: Deogratius Munishi, Oscar Joshua, Nadir Haroub, Simon Msuva, Hartuna Niyonzima, Obrey Chirwa, Yusuf Mhilu
SIMBA SC: Angban, Mwanjale, Lufunga [Juuko], Bakungu, Zimbwe Jumior, Mzamiru, Mkude, Kazimoto, Kichuya, Mavugo [Blagnon], Ajib Mohammed Ibrahim
Akiba: Manyika, Banda, Mohammed, Ndemla, Juuko, Blagnon, Mnyate
REFA: Martin Saanya
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.