Unknown Unknown Author
Title: SHILINGI MILIONI 40 ZA JK ZASHINDWA KUONDOA TATIZO LA X-RAY HOSPITALI YA KIPATIMU.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na. Ahmad Mmow, Kilwa Masoko. Pamoja na nia njema ya Rais msitahafu, Dkt Jakaya Kikwete ya kumaliza tatizo la kipimo cha X-Ray, katika h...
Na. Ahmad Mmow, Kilwa Masoko.
Pamoja na nia njema ya Rais msitahafu, Dkt Jakaya Kikwete ya kumaliza tatizo la kipimo cha X-Ray, katika hosipitali ya Kipatimu. Hadi sasa tatizo hilo halijaondoka na wananchi wanaendelea kukosa huduma hiyo.
Digital X-Ray
Hayo yameelezwa na baadhi ya wananchi wa kata Kipatimu mbele ya mkuu wa wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika hivi karibuni katika kijiji cha Kipatimu.

Wananchi hao wakiongozwa na diwani wa kata hiyo, Imamu Ntenandena, walisema nia njema ya Rais mstahafu, Dkt Jakaya Kikwete ya kuondoa tatizo la X-Ray katika hosipitali ya kanisa katoliki ya Kipatimu yenye uwezo wa kulaza wagonjwa takribani 60, haijazaa matunda.

Wakibainisha kwamba hawajui shilingi milioni 40 zilizolizotolewa na Rais mstahafu huyo mwaka 2012 ili zitumike kutengeneza X-Ray ya hosipitali hiyo zilipo na zinafanyanini.

Renfrida Mtumbuka, licha ya kuomba hosipitali hiyo iongezwe daktari, alisema kukosekana kwa kifaa tiba hicho kunasababisha wasafiri umbali mrefu kwenda hosipitali ya wilaya hiyo iliyopo Kilwa Kivinje.

Wakati Rais msitahafu alishatoa kiasi hicho cha fedha tangu mwaka 2012, ili zitumike kwa matengenezo X-Ray ya hosipatali hiyo inayoendeshwa kwa ushirikiano baina ya halmashauri ya wilaya ya Kilwa na jimbo katoliki la Lindi.

Hata hivyo haijatengenezwa na hawajui fedha hizo zipo wapi nazinafanya kazi gani.

Mwananchi mwingine, Mbaraka Ngwembano, alisema nijambo la kushangaza kuona wanaendelea kupata shida wakati fedha zilishapatikana. Huku akieleza kwamba zipodalili za kupuuza maagizo ya viongozi wa juu kuhusu suala hilo. 

Kwa madai kwamba mkoa uliagiza halmashauri ya wilaya ya Kilwa itoe maelezo ya kwanini fedha hizo hazijatumika na zipo wapi. Hata hivyo wananchi hawajaambiwa chochote na hawajui kinachoendelea. Badala yake wanazidi kuteseka bila kujua mwisho wa mateso hayo.

Nae diwani wakata hiyo, Imamu Ntenandena, ambae alishauri kijengwe kituo cha afya katika kata hiyo badala ya kutegemea hosipitali hiyo. Alisema kama serikali ambayo inasitahili kuheshimiwa na kuogopwa ilitoa fedha kwania njema lakini hakuna kilichofanyika, itakuwa nivigumu kuthaminiwa michango ya wananchi ambao wameamua kuzitatua kero na changamoto kupitia nguvu zao.
"Huenda nikwasababu hosipitali ile niya misheni, basi ni bora tujengewe kituo cha afya na tupo tayari kuchangia kwa hali na mali," alisema Ntenandena.
Kipatimu Hospital
Akijibu kwa niaba ya mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hiyo, mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Kilwa, Dk Vitalis Katalyeba, alikiri kuwa pesa hizo zilitolewa na zipo benki. Ingawa hadi sasa zilizopo ni shilingi 39.4 milioni Kwasababu ya makato ya utunzaji fedha hizo yanayofanywa na benki kwa kipindi chote hadi sasa.

Alisema fedha hizo zilitolewa kwa lengo la kufanyia matengenezo X-Ray mbovu iliyopo. Hata hivyo ilibainika kuwa tatizo la kifaa tiba hicho nikubwa. Isingewezekana kukifanyia matengenezo.
" Kwahiyo ilikubaliwa inunuliwe mpya, hatahivyo kwa wakati huo ilikuwa inauzwa shilingi milioni themanini. Kiasi ambacho hakikuwepo, kwahiyo zikawa zinafanyika juhudi za kutafuta fedha za kuongeza ili iweze kununuliwa," alisema Dk Katalyeba. 

Kwa upande wake, mkuu wa wilaya, Chritopher Ngubiagai, licha ya kushangazwa na kuchelewa kuongezwa fedha hizo na kununua kifaa hicho ili kuokoa maisha ya wananchi. Alisema "Suala la afya sio la kuchezea, tunapojadili na kupanga kuhusu uhai tuache kufanya masihara. Haiingii akilini mtu alitoa fedha lakini hakuna kilichofanyika." Kwakipindi chote hiki mmeshindwa kuongeza ili kuokoa maisha ya watu mnaona sawa tu," alihoji Ngubiagai. 

Mkuu huyo wa wilaya alisema kitendo hicho kinaweza kuwakatisha tamaa wahisani wengine wa maendeleo. Hivyo kunahaja ya kutafuta njia za haraka fedha hizo ziongezwe ili kifaa hicho kikanunuliwe.
"Miaka minne fedha zipo kwenye akaunti zinapungua mnaziangalia tu, aliyetoa atajisikiaje na atatuonaje akisikia hazijatumika na wananchi wanaendelea kuteseka," aliendelea kuhoji.

Licha ya tatizo la X-Ray, hosipitali hiyo inakabiliwa na tatizo la upungufu wa wataalamu. Ambapo hadi sasa inadaktari mmoja na wauguzi watatu tu.
*************

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top