Jina lake halisi ni Christopher Fabian Mashali ila jina la kazi ni maarufu kama Thomas Mashali.
Umaarufu wake umetokana na uwezo wake wa kupigana akiwa ulingoni ambapo amewahi kupigana dhidi ya mabondia mbalimbali wa ndani na nje ya nchi.
Mashali ambaye alikuwa bado anahitajika kwenye tasnia ya ngumi Tanzania amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Mashali ambaye alikuwa bado anahitajika kwenye tasnia ya ngumi Tanzania amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Hadi sasa bado chanzo cha kifo chake hakijulikani huku matukio mchanganyiko yakihusishwa na kifo.
Ripoti ya awali inasema Thomas Mashali amefariki kwa kupigwa na wananchi baada ya kuhusishwa na tetesi wa wizi.
Lakini upande mwingine umedai kuwa Mashali alikuwa kwenye ugomvi binafsi na mtu kabla ya kupigwa na kujeruhiwa eneo la Kimara huku ikielezwa kuwa alikuwa kwenye klabu cha pombe.
Mashali anayedaiwa kuvuja damu nyingi kabla ya kufikishwa hospitali, inasemekana kuwa hadi jioni ya ya jana alikuwa na bondia mwenzake, Francis Cheka.
Mashali anayedaiwa kuvuja damu nyingi kabla ya kufikishwa hospitali, inasemekana kuwa hadi jioni ya ya jana alikuwa na bondia mwenzake, Francis Cheka.
Baada ya tukio hilo la kupigwa huko Kimara Mashali alipelekwa katika Hospitali ya Sinza Palestina kabla ya kupelekwa Muhimbili ambako mauti ilimkuta.
Taarifa zaidi kuhusu msiba huu zinafuata hapahapa.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.