MSANII ALICE KELLA AFUNGUKA KUHUSU MASLAHI YA WASANII KATIKA KAZI ZAO (+VIDEO)

Kumekuwa na malalamiko ya hapa na pale juu ya wasanii kuibiwa kazi zao na wakati mwingine kutumika bila ridhaa zao; jambo hili limekuwa likiwaumiza vichwa wasanii na kuikosesha usingizi serikali kiasi cha kutafuta mbinu mbadala ya kupambana na wizi wa kazi za wasanii ili kuboresha maslahi ya wasanii hao.
Alice Kella
‘Support’ ya kazi za wasanii imeongezeka kuanzia kwa madj, watangazaji na wasanii wenyewe baada ya kutambua thamani ya muziki kama moja ya sekta inayotoa ajira kubwa kwa vijana wa kitanzania. Zamani muziki ulichukuliwa kama uhuni lakini kwa sasa muziki ni ajira.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nauye aliwahi kutoa ahadi kwa kusema atahakikisha wasanii wanafaidika kupitia kazi ya sanaa wanayoifanya.

Alice Kella amepiga stori na Lindiyetu.com nae amegusia ishu ya maslahi ya wasanii na jinsi wanavyopaswa kulipwa, bonyeza hapo chini kumsikiliza akifunguka.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post