MANCHESTER UNITED WAPOKEA KICHAPO CHA 4-0 DHIDI YA CHELSEA STAMFORD BRIDGE

CHELSEA Leo hii wameitandika Manchester United 4-0 Uwanjani Stamford Bridge kwenye Mechi ya EPL, Ligi Kuu England, ambayo ni Mechi ya kwanza kwa Meneja wa Man United Jose Mourinho kurejea Uwanjani hapo tangu afukuzwe Umeneja Chelsea Desemba 2015.
CHELSEA
Man United, wakionyesha ugoigoi mkubwa katika Gemu yote, walikuwa nyuma 2-0 hadi Mapumziko na Chelsea walipata Bao lao la kwanza Dakika ya Kwanza tu Mfungaji akiwa Pedro.

Bao la Pili la Chelsea lilifungwa na Gary Cahill.

Kipindi cha Pili, Chelsea walipiga Bao nyingine 2 kwenye Dakika za 62 na 70 Wafungaji wakiwa Eden Hazard na Ngolo Kante.

CHELSEA
Matokeo haya yamewaweka Chelsea Nafasi ya 4 wakati Man United wanabaki Nafasi ya 7.

VIKOSI: Chelsea: Courtois; Azpilicueta, David Luiz, Cahill; Moses, Kante, Matic, Alonso; Pedro [Chalobah, 71’], Hazard [Willian, 78’] Diego Costa [Batshuayi, 78’]
Akiba: Begovic, Aina, Terry, Chalobah, Oscar, Willian, Batshuayi.

Manchester United:
De Gea; Valencia, Bailly [Rojo, 52’], Smalling, Blind; Herrera, Fellaini [Mata, 45’], Lingard [Martial, 65’], Pogba, Rashford, Ibrahimovic.
Akiba: Romero, Rojo, Darmian, Carrick, Young, Mata, Martial.

REFA: Martin Atkinson

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post