Unknown Unknown Author
Title: BAADA YA KUTWAA TUZO HARMONIZE ANENA HAYA. (+VIDEO)
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Siku ya jana furaha ilienea katika kila nyuso ya mpenda burudani wa Tanzania hasa kwa wale mashabiki wa lebo ya muziki ya WCB Wasafi . N...
Siku ya jana furaha ilienea katika kila nyuso ya mpenda burudani wa Tanzania hasa kwa wale mashabiki wa lebo ya muziki ya WCB Wasafi.
Harmonize
Ni baada ya wasanii wawili kutoka katika lebo hiyo kuweza kushinda tuzo za AFRIMMA zilizokuwa zikitolewa alfajiri ya jana huko Dallas Texas Marekani.

Ni Diamond Platnumz ambaye alishinda tuzo ya Best Male East Africa pamoja na Harmonize ambaye alishinda Best New Comer Africa. Mtanzania mwingine aliyeshinda tuzo ni Dj D Ommy kutoka Clouds Media Group.

Ni Harmonize pekee ndiye ambaye alikuwepo eneo la tukio wakati tuzo hizo zikitolewa na hivyo kuweza kumuwakilisha Diamond Paltnumz ambaye alikuwepo katika shughuli zingine.

Lindiyetu.com imepiga story na Harmonize na kujua anajiona wapi, na anajipanga vipi baada ya kushinda tuzo hiyo.
“Nimefurahi kwasababu hii ndio mara yangu ya kwanza kushinda tuzo tangu nimeanza muziki, tuzo hii inanipa motivation na kunifanya nifanye kazi kwa bidii kwasababu bado naamini safari ni ndefu sana. Lakini naweza kusema tuzo hii imenifungulia milango na nizidi kuamini kuwa muziki wangu unafika mbali zaidi. Namshukuru mwenyezi mungu na pia wote ambao mmenipigia kura.” Alisema Harmonize.

Harmonize hakuishia hapo tu, yapo mengi sana ambayo ameyazungumza. Full interview nimekuwekea hapa chini kwenye hii video unaweza kuitazama.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top