NDEGE BINAFSI YA CRISTIANO RONALDO YAANGUKA

Ndege binafsi ya mchezaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ilianguka wakati ikitua kwenye uwanja wa ndege wa El Prat jijini Barcelona, Jumatatu. Hakuna majeruhi walioripotiwa.
Ronaldo Plane
Kwa mujibu wa ESPN, Ronaldo, aliyekuwa Dortmund kipindi hicho wakati Real Madrid ilikuwa ikijiandaa kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa waliotoka sare ya 2-2 katika hatua ya makundi dhidi ya Borussia Dortmund, hakuwa ndani ya ndege hiyo wakati inaanguka.

Mshambuliaji huyo huikodisha ndege hiyo, Gulfstream G200, aliyoinunua kwa €19m kufanya kazi zingine wakati asipokuwa akiitumia.

Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari vya Hispania, matairi ya magari hayo yalivunjika wakati ikitua na hivyo kutoka nje ya njia.

********************************************
IPAKUE NYIMBO MPYA YA SAM WA UKWELI "KISIKI" IKIWA NI MAHADHI YA CLUB

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post