Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Aron Kagurumjuli amevunja Baraza la Madiwani rasmi baada ya serikali kuigawa manispaa hiyo kuwa mbili.
Alipokuwa akitangaza kulivunja baraza hilo, Kagurumjuli alisema amevunja baraza hilo kwa kuwa serikali imegawanya manispaa hiyo kuwa wilaya mbili, ya Kinondoni na Ubungo hivyo kwa kuwa wilaya zote tayari zina wakurugenzi, wakuu wa wilaya na makatibu tawala wa wilaya imempasa kufanya hivyo.
“Baraza la madiwani limevunjwa, kuvunjwa kwa baraza hili ni ukomo wa meya pia,” alisema.
Katika baraza hilo lililovunjwa UKAWA walikuwa na viti vya Udiwani 38 (CHADEMA 29 na CUF 9), huku CCM wakiwa na viti 15 tu.
ALIYEKUWA MEYA WA KINONDONI BONIFACE YAKOB
Kagurumjuli alilivunja juzi saa 11:00 baada ya kumalizika kwa Baraza la Madiwani la kawaida.
Alipokuwa akitangaza kulivunja baraza hilo, Kagurumjuli alisema amevunja baraza hilo kwa kuwa serikali imegawanya manispaa hiyo kuwa wilaya mbili, ya Kinondoni na Ubungo hivyo kwa kuwa wilaya zote tayari zina wakurugenzi, wakuu wa wilaya na makatibu tawala wa wilaya imempasa kufanya hivyo.
“Baraza la madiwani limevunjwa, kuvunjwa kwa baraza hili ni ukomo wa meya pia,” alisema.
Katika baraza hilo lililovunjwa UKAWA walikuwa na viti vya Udiwani 38 (CHADEMA 29 na CUF 9), huku CCM wakiwa na viti 15 tu.
Katika mgawanyo uliotokea madiwani 18 wa UKAWA watakuwa kwenye halmshauri mpya ya UBUNGO. na 20 halmashauri ya KINONDONI. Huku CCM madiwani 7 UBUNGO na 8 KINONDONI.
Aliongeza kuwa wiki ijayo kutakuwa na uchaguzi wa meya katika manispaa hizo.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni aliyekuwepo kabla ya kuvunjwa kwa baraza hilo ni Boniface Yakob ambaye amebaki nafasi yake ya udiwani.

Kuvunjwa kwa baraza hilo kulikuwa kunatarajiwa baada ya serikali kugawanya manispaa ya Kinondoni kuwa mbili.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.