“Muziki wa dansi ni muziki wa starehe na siyo ugomvi baina ya sisi wanamuziki, ndiyo maana bado nawasiliana na akina Nyoshi El Saadat, Khalid Chokoraa na Kalala Junior japokuwa sifanyi nao kazi kwasasa ila bado ni marafiki na ndugu zangu wa karibu.
“Nawaomba wanamuziki wenzangu wote nchini tuungane kuuinua muziki huu ambao kwa siku za hivi karibuni upinzani kutoa aina nyingine za muziki umekuwa mkubwa. Ukigeuka huku kuna Bongo fleva, huku taarabu kule kuna singeli lazima sasa wanamuziki wa dansi tukae chini na tujipange kuhakikisha tunauinua muziki wetu.
“Namshukuru mama yetu ambaye pia ni mmiliki wa bendi ya Twanga Pepeta (African Stars Band) ambaye amejitolea kuuinua tena muziki wetu kwa kutoa zawadi ya pesa taslimu kwa waandishi wote watakaokuwa vinara kuutangaza muziki huu wa dansi nchini, ni wakati sasa sisi wanamuziki tutunge nyimbo nzuri zitakazokidhi mahitaji ya mashabiki wetu kama zamani.”
_______________________________________
TAZAMA HAPA SHOW YA USIKU WA VIGOMA JIJINI TANGA, WEMA SEPETU AKIKATA MAUNO.
TAZAMA HAPA SHOW YA USIKU WA VIGOMA JIJINI TANGA, WEMA SEPETU AKIKATA MAUNO.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.