HABARI ZA HIVI PUNDE:: MSAFARA WA MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA SULUHU HASSANI WAPATA AJALI NANGURUWE-MTWARA

Ajali mama samia
Msafara wa makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Samia Suluhu Hassani ambao ulikuwa unaelekea wilayani Tandahimba ukitokea ikulu ndogo ya Rais Mtwara umepata ajali na kusababisha majeruhi ambao wamekimbizwa hospitali ya rufaa ligula.
Ajali mama samia
Ajali imetokea mbele kidogo ya kijiji cha Nanguruwe kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara

Majeruhi walioumia ni dereva pamoja na wasaidizi wanne wa Makamu Rais.

Ajali mama samia
Awali kabla ya gari hilo lililobeba wasaidizi wa rais kuacha njia na kupinduka, gari liliokuwa limebeba waandishi wa habari wa Channel Ten, Startv na Clouds Tv liliacha njia na nusura kupinduka.
___________________________________________________
ITAZAME HAPA VIDEO MPYA YA MALAIKA - RARUA KISHA TOA MAONI YAKO

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post