Gavana wa BOT, Prof. Benno Ndulu
Kitendo hicho kimewafanya watu wa kada mbalimbali na wananchi kwa ujumla kulalama hali ya maisha kuzidi kuwa ngumu kiasi cha kusema pesa zimeadimika hali iliyomfanya Rais Magufuli kusema “watasema hela imepotea … nafahamu ‘trend’ ya watu wanavyohamisha hela kutoka benki kwenda kuficha”.
Akasisitiza “Naweza nikaamua hata siku mbili tatu nikabadilisha hela ili hela walizoficha kwenye magodoro zikaozee huko huko, ni nafuu wazichukue na kuzipeleka kwenye mzunguko zikafanye kazi wajenge uchumi”.
Sasa taarifa iliyopo kwa sasa ni juu ya Benki Kuu ya Tanzania kuvunja ukimya kuhusu hali ya uchumi nchini ambapo Gavana wa BOT, Prof. Benno Ndulu, kusema hali ya uchumi nchini imeendelea kuimarika kwani Tanzania ni kati ya nchi kumi Afrika ambazo uchumi wake unakuwa vizuri ambapo katika robo ya kwanza ya mwaka huu kasi ya ukuaji wa pato la taifa imefikia asilimia 5.5 ikilinganishwa na ongezeko la asilimia 5.7 ya kipindi kama hicho mwaka 2015.
Prof. Ndulu amesisitiza mapato bandarini yameendelea kudhibitiwa na kuongezeka licha ya mizigo kupungua huku akiba ya fedha za kigeni ikiwa ni dola bilioni 4 ambapo amesisitiza juhudi za kuendelea kudhibiti matumizi zimefanyika na kufanya bajeti ya mwaka 2016/17 kutekelezeka bila shida.
Kuhusu tuhuma zinazoenea juu ya baadhi ya watu kuficha fedha na kufanya mzunguko wa fedha kuwa mgumu Prof. Ndulu amesema“fedha nyingi zilizokuwa zikitumika vibaya zimerudi zinasaidia umma moja kwa moja na sio maana yake unawagawia hapana, kama ni elimu, kujenga madarasa, madawati na vitu hivi vyote bado kuna watu watapata shughuli ya kufanya”.

_______________________________________
TAZAMA HAPA SHOW YA USIKU WA VIGOMA JIJINI TANGA, WEMA SEPETU AKIKATA MAUNO.

Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.