WAZIRI NAPE AISHAURI NSSF KUWEKEZA LINDI, IKIWEMO UWANJA WA NANE NANE - NGONGO

NSSF NANE NANE LINDI 1
Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo Nape Nnauye (wakwanza kushoto) ishauri NSSF kuwekeza Mkoani Lindi Ikiwemo Uwanja wa Nane nane Ngongo, ameyasema hayo leo hii alipotembelea Banda la NSSF lililopo viwanjani hapo katika maonyesho hayo ya wakulima yanayofanyika Kitaifa mkoani Lindi. 
Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Ndg Godfrey Zambi na wakwanza kulia ni Salimu Khalfani Kimaro ambaye ni Afisa Mkuu mwandamizi Idara ya Masoko na Mahusiano NSSF. 
NSSF NANE NANE LINDI 2
Wananchi wakipata Maelekezo ya Huduma zitolewazo na NSSF katika Viwanja hivyo vya Nane nane Ngongo.  
NSSF NANE NANE LINDI 3
Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo Nape Nnauye (wakwanza kushoto) akiendelea kupata maelekezo ya huduma zitolewazo katika banda hilo na NSSF.
NSSF NANE NANE LINDI 4
Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo Nape Nnauye akiweka sahihi katika Daftari la wageni kushoto ni Salimu Khalfani Kimaro ambaye ni Afisa Mkuu Mwandamizi Idara ya Masoko na Mahusiano NSSF.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post