Unknown Unknown Author
Title: JOSE CHAMELEONE AFUNGUKA KUHUSU KUWA NA BIFU NA DIAMOND AMEYASEMA HAYA...
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Msanii mkongwe wa muziki nchini Uganda,  Jose Chameleone amekanusha uvumi ulioenea kuwa yeye ana bifu na msanii wa bongo fleva,  Diamond P...
Msanii mkongwe wa muziki nchini Uganda, Jose Chameleone amekanusha uvumi ulioenea kuwa yeye ana bifu na msanii wa bongo fleva, Diamond Platnumz.
Chameleone and Diamond
Akihojiwa na William Tuva wa kipindi cha Mseto, nchini Kenya Chameleone amedai kuwa media zinajaribu kuchochea bifu yake na Diamond lakini yeye hana sababu yoyote ya kuwa na ugomvi na nyota huyo wa Tanzania.
“Unajua watu wamejitahidi sana kuweka line za bifu kati yangu na Diamond..unajua nilikuwa kwenye Tv Show moja Kampala nikaulizwa maswali fulani kuhusu Diamond lakini media wenyewe wakabadilisha hayo maneno yawe maneno ya kumtukana Diamond.It is very ashaming,kwa sababu mimi katika tour yangu ya USA niliongea na Diamond pamoja na Babu Tale,i respect him as an artist.i have reason to say bad things about him” 
Alifunguka Chameleone ambaye kwa sasa yuko nchini Kenya kwa ajili ya kushiriki Coke studio.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top