HATIMAE SHAMSA FORD AMUWEKA HADHARANI MPENZI WAKE MPYA NA TAYARI KASHATOA MAHARI

Msanii wa filamu Shamsa Ford amemuweka wazi mpenzi wake aliyekuwa akimficha kwa muda mrefu usiku wa siku yake ya kuzaliwa huku akimtupia Mama yake mzazi shukurani za kutosha.
Shamsa Ford
Akiongea na Enewz ya East Africa Television Jumatatu hii, Shamsa amesema baada ya kutendwa mara kadhaa alikuwa anaogopa kuweka wazi mahusiano yake.
“Nakuwaga mzito labda kwa sababu ya uwoga lakini mapenzi yakikuzidi mwisho wa siku unashindwa kujizuia, ni kweli nimetolewa mahari,” alisema Shamsa.
Shamsa Ford
Pia muigizaji huyo amemwagia sifa mama yake mzazi huku akimshuru kwa malezi mazuri ambayo yamemfanya aonekane mtu mbele ya watu.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post