Askari akiwa amewakamata Viongozi wawili wa Serikali ya Kijiji waliokuwa wakituhumiwa kwa ubadhirifu wa viwanja.
Mkuu wa Idara ya Ardhi na Maliasili Ndugu Japhet Muogopeni Mnyagala akizungumza mbele ya Wananchi .
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mhe. Juma Zuberi Homera akizungumza na Wananchi wa Vitongoji vya Frank Weston na Umoja vilivyokumbwa na mgogoro wa ardhi.
Mkuu wa Wilaya Tunduru Mhe. Juma Zuberi Homera akimuagiza Mkuu wa Idara ya Ardhi na Maliasili Ndugu Japhet Muogopeni Mnyagala kuchukua hatua stahiki kuhusiana na mgogoro wa Ardhi ndani ya Wilaya hiyo.
Wananchi wakimsikiza kwa makini Mhe DC. Juma Zuberi Homera .
Mkuu wa Wilaya Tunduru Mhe. Juma Zuberi Homera, amewatia mbaroni Viongozi wanne wa Serikali ya vijiji kwa kosa la usimamizi mbovu wa ardhi katika Vitongoji vya Umoja na Frank Weston katika kata ya Nanjoka Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma.
Akisoma taarifa mbele ya Mkuu wa Wilaya Bw. Yahaya Issa Abdallah alimueleza DC. Homera kuwa Vitongoji vya Umoja na Frank Weston vimekumbwa na mgogoro wa ardhi kati ya Wenyeji, Wageni na Wafanyakazi wa Halmashauri ya Wilaya Tunduru kwa muda mrefu.
Aidha Serikali kupitia Idara ya Ardhi na Maliasili Wilaya, iliwapimia ardhi Wananchi toka 11/08/2014 lakini ikabainika kuwa mpaka 30/06/2016 bado Wananchi hawakupewa maeneo yao na kuna baadhi ya Wafanyakazi wa Halmashauri pamoja na Wageni wapo kwenye orodha ya Wananchi wanaopaswa kugawiwa Viwanja.
Akihutubia kwenye mkutano huo wa hadhara, uliyofanyika katika Shule ya Msingi Umoja, DC Homera aliwaeleza Wananchi kuwa wasiwe na shaka, kwa sababu Serikali ipo upande wao na hakuna atakaye dhurumiwa haki yake, alisema
“Namtaka Mhasibu wa Ardhi na Maliasili alete orodha ya waliolipia Ardhi maeneo ambayo siyo ya wakazi, na ambao ni Watumishi wa Halmashauri wafutwe kwenye orodha hiyo na warejeshewe fedha zao”.Mfano, kuna baadhi ya watumishi wa Idara ya Ardhi na Maliasili, ambao wamefanya ujanja ujanja kinyume cha sheria kwa kuwaweka watoto wao kwenye orodha, na majina yao yameorodheshwa hapa, hivyo hatua za kisheria na taratibu zitafanyika kuondoa huu mgongano ambao umejitokeza katika hili pia.
Kama vile haitoshi ikabainika kuwa kuna baadhi ya Viongozi walikusanya fedha za wananchi wapatao 522 na kutowapa risiti, jambo amablo ni hujuma za wazi kabisa za kuikosesha Halmashauri ya Tunduru Mapato na kupelekea fedha kuwa mikononi mwa wajanja wachache.
Aidha aliwataka Wafanyakazi wa Idara ya Ardhi na Maliasili kujieleza ni kwa nini wamewagawia watu ardhi ambao sio wakazi? kwa nini wamefanya udanganyifu wa kuwa milikisha ardhi Watumishi wa Halmashauri kwa njia za rushwa? na kwa nini wananchi zaidi ya 522 hawajapewa maeneo yao kwa zaidi ya Miaka Miwili?
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Ardhi na Maliasili wa Wilaya ndg. Japhet Muogopeni Mnyagala alikiri kufanya kosa, lakini pia alimuakikishia Mkuu wa Wilaya ndani ya wiki moja wananchi wataanza kugawiwa viwanja na zoezi hilo litaanza Kesho (leo).
Mkuu wa wilaya aliwaagiza askari wakamate viongozi walio kuwa wasimamizi wa upimaji wa maeneo katika vitongoji vya Umoja na Frank Weston ambao ni Mohammed Dumsala, Matola Limelime, Halid Daud na Tekla Damas.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.