Timu ya Kata ya Mnazi Mmoja leo hii imeikaribisha Timu ya Kata ya Mtanda A katika dimba la uwanja wa Ilulu katika muendelezo wa Ligi ya RPC ndani ya Manispaa ya Lindi.
Anafi Jamvi aliweza kuipatia timu yake goli la kufutia machozi baada ya kupokea cross kutoka kwa winga wa kulia na kumpita golikipa na kuutupia mpira kimiani.
Katika Mchezo huo Mtanda ilijikuta ikipata kipigo cha paka mwizi cha Magoli 4 - 1.kutoka kwa Timu hiyo ya Kata ya Mnazi Mmoja yenye maskani yake nje kidogo ya Mji wa Lindi Takribani kama Kilometa 25 kutoka Mjini.
Hakika wameonyesha kuwa hawakuja kushangaa Majukwaa ya Uwanja wa Ilulu bali kutafuta pointi tatu muhimu kwani iliwachukua dakika 14 tu kupata bao la kwanza kupitia kwa mshambuliaji wao Abdallah Ismail.

Dakika 5 baadae Hamisi Nangomwa aliweza kudhirisha umahiri wa Safu ya ushambuliaji ya timu hiyo kuwa iko vizuri pale alipoiandikia timu yake bao la pili mnamo dakika ya 19 ya mchezo katika kipindi cha kwanza.
Mnazi Mmoja waliendelea Kuonyesha Kandanda Safi na kuweza kuwapa burudani ya kutosha mashabiki lukuki waliohudhuria mechi hiyo jioni ya leo na kivutio kikubwa kikiwa ni winga wake machachari Hashimu Hamisi a.k.a D7 aliyefananishwa na Christiano Ronaldo anayekipiga kule Hispania katika Timu ya Real Madrid.
Kudhihirisha kuwa Hawakukosea kumpa jina hilo la D7 Mnamo dakika ya 38 aliweza kuwachambua mabeki na goli kipa na kuweka mpira kimiani na kuihakikishia timu yake ya Mnazi Mmoja kuwa inaondika na Point Tatu muhimu katika mchezo huo.
Anafi Jamvi aliweza kuipatia timu yake goli la kufutia machozi baada ya kupokea cross kutoka kwa winga wa kulia na kumpita golikipa na kuutupia mpira kimiani.
Hadi Dakika 45 za Kipindi cha Kwanza zinamalizika Mtanda A 1 - Mnazi Mmoja 3.
Kipindi cha pili kilianza kwa Timu ya Mtanda A kuonesha kuwa walizidiwa maarifa, walianza kucheza rafu nyingi dhidi ya wapinzani wao lakini vijana wa Mnazi Mmoja waliweza kuwasoma kimchezo na kucheza kwa tahadhari sana na dakika ya 88 Hashimu Hamisi D7 alipachika bao lake la pili katika mchezo huo na la nne kwa timu yake na likawa ndilo goli la ushindi wa Mechi hiyo hadi kipyenga cha mwisho cha Muamuzi.

Aidha Kabla ya Mechi hiyo Awali kulikuwa na Mchezo wa Kundi B ambapo timu za Polisi na Matopeni zilitoka Suluhu ya goli 1-1.
Goli la Polisi likifungwa na Ahmeid Fakhi dakika ya 36 ya mchezo huku lile la Matopeni likifungwa na Mussa Ngalaga Mnamo dakika ya 42.
Hata hivyo Timu ya Matopeni walicheza pungufu, hiyo ilikuja baada ya Mohamed Machelenga kuzawadiwa Kadi nyekundu na mwamuzi wa Mchezo huo mnamo dakika ya 30 ya kipindi cha Kwanza.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.